Home » » CCM Tabora yawasaidia waendesha Bodaboda

CCM Tabora yawasaidia waendesha Bodaboda

CHAMA cha Mapinduzi Mkoani Tabora kimewasaidia waendesha Pikipiki maarufu kama boda boda jumla ya pikipiki Saba ili kuimarisha umoja wao katika manispaa ya
Tabora.

Mchango huo umetolewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika mkutano wa uzinduzi wa Katiba mpya ya chama cha waendesha Bodaboda katika Manispaa ya Tabora.

Mwenyekiti wa  wa CCM Mkoa wa Tabora,Bw. Hassan Wakasuvi, amewapongeza kwa jitihada zao waendesha bodaboda kwa uamuzi wa kuunda umoja utakaowasaidia kuratibu mambo yao ikiwemo kutatua matatizo mbalimbali yatakayowakabili katika shughuli zao.

Amewataka vijana hao kutambua kuwa kuendesha Bodaboda
ni kazi kama ilivyo kazi zingine, hivyo akawaasa kuwa na maadili mema
wawapo kazini hasa katika uvaaji, sanjali na kuiheshimu kazi yao na
kuzingatia utiifu wa sheria zote za usalama barabarani ili kujiepusha
na ajali za kujitakia ambazo zinaangamiza maisha yao kila siku kutokana na uzembe

Akizindua umoja huo , Wakasuvi amesema  jitihada
za vijana hao ni za kimaendeleo na zinafaa kuungwa mkono na wapenda
maendeleo wote ambapo makada mbalimbali waliwachangia na kupatikana Pikipiki saba na pesa taslimu zaidi zaidi ya shilingi laki tatu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa