Jumuia ya Umoja Wazazi Tanzania
wametakiwa kuishauri serikali kusimama katika nia yake ya kurejesha adhabu ya
viboko mashuleni ili kuboresha nidhamu kwa wanafunzi ambayo imekuwa ikimomoyoka
siku hadi siku.
Mwenyekiti
wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora Bw, Moshi Omary, ameitaka jumuia
ya wazazi hapa nchini kuindikia barua rasmi ya kuiomba serikali iweke mkazo
katika kurejesha adhabu ya
viboko shuleni.
Bw,
Omary amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza nidhamu shuleni na kupunguza
vitendo vya kihuni miongoni mwa wanafuni.
Kwa upande wake
mjumbe wa baraza kuu la wazazi Taifa Bw. Kajoro Vyohoroka, Amekitaka Chama cha
(CCM) kutoa nafasi sawa za uwakilishi kwa jumuia zake katika nafasi za maamuzi
kama ujumbe wa Nec na Ubunge.
Mjumbe
huyu wa jumuia hiyo amesema ccm imetoa nafasi nyingi za ujumbe wa Nec na Ubunge
kwa jumuia za vijana na wanawake na kuisahau jumuia hiyo.
0 comments:
Post a Comment