Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora
Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza
na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa
kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano
hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi.tolle
Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa
Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki
Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni
zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa
Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia
Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa
kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa
shindano hilo.
Meya wa Manispaa ya Tabora
katikati Akimkabidhi kiongozi wa kundi la Mwenge fedha tasilimu
shilingi laki sita mara baada ya kundi hilo kutangazwa Washindi wa shindano
la ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora ambalo limefadhiriwa na kampuni ya
Bia Tanzania Tbl kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Meneja
matukio wa kampuni hiyo kanda ya Ziwa Bw Eric Mwayela.
HATIMAYE FAINALI ZA MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KWA MKOA WA TABORA
AMBAYO YAMEDHAMINIWA NA KAMPUNI YA BIA TANZANIA-TBL KUPITIA BIA YAKE YA
BALIMI EXTRA YAMEMALIZIKA RASMI KWA KUNDI LA MWENGE KUIBUKA BINGWA WA
MASHINDANO HAYO NA KUJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI LAKI 6 NA HIVYO
KUPATA TIKETI YA KUUWAKILISHA MKOA HUO KATIKA MASHINDANO YA KANDA
YATAKAYO FANYIKA JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNI.
KATIKA
KINYANG'ANYILO HICHO
AMBACHO KIMEVUTA HISIA ZA WAKAZI WENGI WA MKOA HUO, KUNDI HILO
LIMEIBUKA MSHINDI KWA ALAMA 90 LIKIFUATIWA NA KUNDI LA MAGEREZA AMBAYO
IMEPATA ALAMA 87 NA KUONDOKA NA ZAWADI YA SHILINGI LAKI 5 HUKU NAFASI YA
TATU IKICHUKULIWA NA MASANGE JKT AMBAO WAMEJINYAKULIA SHILINGI LAKI 400
KWA KUPATA ALAMA 77, NAFASI YA 4 IMECHUKULIWA NA KUNDI LA MWAMKO
SIKONGE NA KUJIPATIA SHILINGI LAKI 3KWA KUPATA ALAMA 63.
KATIKA
MPAMBANO HUO AMBAO UMEVISHIRIKISHA VIKUNDI 10 WASHIRIKI WOTE KUANZIA
NAFASI YA 5 MPAKA YA 10 WAMEJINYAKULIA ZAWADI YA FEDHA TASILIMU SHILINGI
LAKI MOJA NA NUSU HUKU MEYA WA MANISPAA HIYO MSTAHIKI MEYA GULAMHUSSEIN
REMTULLAH AMBAYE NDIYE ALIYE KUWA MGENI RASMI AKIIPONGEZA KAMPUNI HIYO
KWA KUDHAMINI MASHINDANO HAYO AMBAPO KUPITIA MASHINDANO HAYO JAMII
IMEKUWA IKIJIKUMBUSHA TAMADUNI ZETU.
GULAMHUSSEIN AMESEMA KUTOKANA NA KAMPUNI HIYO KUFANYA MASHINDANO HAYO KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAVUNO HII
INADHIRISHA KWAMBA BIA HIYO YA BALIMI EXTRA INAMJALI NA KUMSAMINI MKULIMA WA KITANZANIA.
AIDHA
MEYA HUYO AMELITAKA KUNDU HILO LA MWENGE KWENDA KUUWAKILISHA VYEMA MKOA
WA TABORA NA KUHAKIKISHA KUWA WANALEJEA NA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA
KANDA AMBAYO YANATALAJIA KUFANYIKA JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNI.
AWALI
MENEJA WA MATUKIO WA KANDA YA ZIWA BWANA ERICK MWAYELA AMESEMA KUWA
KAMPUNI YAKE KUPITIA BIA YA BALIMI EXTRA WANAJISIKIA FAHARI KUDHAMINI
MASHINDANO HAYO AMBAPO AMEFAFANUA KUWA KUPITIA MASHINDANO HAYO WATU
WAMEKUWA WAKIFAHAMIANA NA KUKUMBUKA NGOMA ZA ASILI ZA MAKABILA YETU.
MASHINDANO
MENGINE KAMA HAYO YANATALAJIWA KUFANYIKA MJINI SHINYANGA MWISHONI MWA
WIKI IJAYO AMBAPO VIKUNDI MBALIMBALI VYA MKOA HUWA VITAPATA FULSA YA
KUSHIRIKI KATIKA MPAMBANO HUO NA HIVYO KUWATAKA WAKAZI WA MKOA HUO
KUJITOKEZA KWA WINGI ILI KUSHUHUDIA MWAKILISHI WAO KATIKA MASHINDANO YA
KANDA.
0 comments:
Post a Comment