MAMLAKA ya Chakula na Dawa Nchini
(TFDA) Kanda ya Magharibi na Kati, imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya
binadamu, zenye thamani ya sh milioni 3.2.
Uteketezaji bidhaa hizo
ulifanyika mkoani hapa baada ya kufanyika ukaguzi maalumu kwa wiki mbili kwenye
maduka ya dawa, majengo, bohari ya dawa na maeneo mengine muhimu.
Akizungumza na waandishi wa
habari eneo la kuteketeza bidhaa hizo, Mkaguzi Kanda ya Kati na Magharibi, Abel
Deule, alisema ukaguzi huo ulihusisha wataalamu kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Tabora na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na ukaguzi huo ulihusisha
biashara ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
Deule aliongeza majengo 192
yalikaguliwa ili kuthibitisha usafi wake, usajili na vibali vya kufanyia
biashara vinavyotolewa na TFDA.
Aliongeza kuwa ukaguzi huo pia
ulijikita zaidi kuangalia ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa
tiba uwepo vifaa bandia zenye viwango duni na uwepo vipodozi vyenye viambata
vyenye sumu.
Deule alibainisha kuwa katika
ukaguzi huo wamebaini kuwa licha ya wafanyabiashara hao kuwa na uelewa, bado
wamekuwa wakiuza vipodozi vyenye viambata vyenye sumu vilivyozuiliwa kuuzwa na
kutumika nchini kwa mujibu wa kifungu namba 88 (a) cha sheria ya chakula, dawa
na vipodozi namba 1 ya mwaka 2003.
Alisema bidhaa zilizokamatwa na
kuteketezwa ni chakula tani 0.129 cha thamani ya sh 775,000, vipodozi
vilivyoisha muda wa matumizi na vyenye viambato vyenye sumu tani 0.245 vya
thamani ya sh 2,298,400 na dawa za binadamu tani 0.001 zenye thamani ya sh
158,000.
Katika
ukaguzi huo, yalipatikana maziwa bandia ya watoto aina ya Lactogen namba
1 na 2 na NAN ambayo ni bandia, dawa ya chanjo ya mifugo ya Newcastle (1-2) iliyositishwa
kuuzwa, dawa bandia aina ya Doxycycline Capsules gramu 100, na pombe kali
iitwayo Shujaa gin ambayo haijapata usajili toka mamlaka ya chakula na dawa.MAMLAKA ya Chakula na Dawa Nchini

iitwayo Shujaa gin ambayo haijapata usajili toka mamlaka ya chakula na dawa.
0 comments:
Post a Comment