Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwasisitizia wahitimu na wageni (hawako
pichani) waliofika katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha
Ufugaji Nyuki Tabora kuwa serikali lazima ijenge Chuo KIkubwa Cha
Ufugaji Nyuki Tabora.
…………………
Na Tulizo Kilaga, Tabora
SERIKALI
imeahidi kujenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufugaji nyuki katika eneo
la Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora ili kuhakikisha
Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika katika uzalishaji wa mazao
yatokanayo na nyuki.
Ahadi
hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda
aliyekuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha
Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora alipokuwa akiwahutubia wahitimu kabla ya
kuwatunuku vyeti na zawadi.
Mhe.
Pinda alisema pamoja na mapungufu ya chuo hicho yaliyotokana na tabia ya
kuhamisha mafunzo yake mara kwa mara kwenda kwenye vyuo mbalimbali vya
Wizara ya Maliasili na utalii nchini, chuo kina umuhimu mkubwa kutokana
na kuwa ni chuo pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa
Afrika.
“Siku
za nyuma chuo kiliweza kupata watu kutoka nchi za nje kuja kujifunza,
hivyo serikali haiwezi kukiacha solemba! Kama tumeweza kujenga Chuo
kikubwa cha Serikali za Mitaa, Hombolo kinachotufanya tushindwe kujenga
chuo kikubwa hivi ni nini? Kwamba hatuoni thamani yake? Si kweli, miaka
kumi ijayo thamani yake itaonekana tu,” alisema Mhe. Waziri Mkuu.
Aliongeza
kuwa, tatizo la kutoendelezwa kwa chuo hicho wakati mwingine kunatokana
na viongozi kutojua kinachoendelea, hivyo aliomba uongozi kuwakilisha
mpango mkakati wake ili serikali iweze kuipembua na kuona wapi pakuanzia
0 comments:
Post a Comment