Home » » Baraza la watoto wenye ulemavu kufanya msako

Baraza la watoto wenye ulemavu kufanya msako



Tabora
BARAZA la watoto wenye ulemavu Mkoani Tabora litaanzisha msako wa nyumba kwa nyumba kuwabaini watoto wenye ulemavu waliofichwa na wazazi na walezi wao.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza,Mwanafunzi wa shule ya msingi Furaha,Glory John,amesema msako huo watauanza hivi karibuni na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Glory ambaye ni mlemavu asiyeona,amesema wanafanya msako huo kwa vile walemavu nao wana haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa wale wasio na ulemavu.
Mwezeshaji wa mabaraza ya watoto wenye ulemavu Nchini,Josephat tonner,amesema mabaraza ya watoto ni muhimu kwa vile watafahamu haki zao na kuzipigania.
Naye mwenyekiti wa kamati ya Ulezi ya baraza la watoto Bi Anna Gelle,amesema watahakikisha wanawasaidia watoto wenye ulemavu na baraza kupaza sauti ili watimiziwe mahitaji yao yaliyo haki yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa