Home » » AJALI YAUA WATATU TABORA

AJALI YAUA WATATU TABORA



Mwili wa kijana mmoja 
aliyefahamika kwa jina la
 Rashidi Seleman mkazi
 wa Isevya manispaa ya
 Tabora ambaye amepoteza
 maisha baada ya Lori walilokuwa
 wamepanda kuanguka eneo la
 Inala barabara ya kwenda 
Kigwa,Polisi wamesema chanzo 
cha ajali hiyo ni mwendo
 kasi wa dereva ambaye 
amekimbia huku watu
 wengine wanne wakiwa 
wamejeruhiwa vibaya ambao 
wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti ya mtu huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali ya kampuni ya mkandarasi JOSSAM


Awali jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki wakiiangalia maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea majira ya saa kumi jioni hapo jana.

Askari wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi....Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX

CHANZO:Mdodosaji

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa