Na Moses
Mabula, Nzega
Mahakama Kuu Kanda ya
Tabora imewahukumu watu watatu kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia
ya kumuua kwa makusudi mkazi wa Kijiji cha Mbagwa wilayani Nzega mkoani
Tabora,Mganga Mgisha, ili mmoja wa wauaji hao apate fursa ya kuoa mke wa
marehemu huyo.
Katika kesi hiyo,
mmoja wa wauaji hao, Kulwa Makomelo alikuwa na njama za kutaka kumuoa mke wa
marehemu huyo,Catherine John, ambapo ilidaiwa alimlipa kiasi cha sh. 20,000
muuaji mwenzake, Kisena Lutonja, ili amsaidie kufanikisha mauaji hayo.
Mke wa marehemu huyo
ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu hiyo. Akitoa hukumu hiyo iliyochukua muda
wa saa tatu, Jaji Amiri Mluma, alisema mahakama imeridhika na ushahidi
uliotolewa kuwa washtakiwa hao walipanga mauaji hayo.
Alisema washtakiwa wamepatikana
na shtaka hilo la kupanga kuua na kufanya mauaji."Walipanga makusudi kumuua
Mugisa, hivyo mahakama inawahukumu kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa
watu wengine.
Jaji huyu aliiambia
mahakama hiyo kwamba; "Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya watu
kushambuliana kwa mapanga bila sababu na kujichukulia sheria mkononi natoa
adhabu hii ili iwe fundisho kwa watu wa aina hiyo."
Awali, mwanasheria wa Serikali,
Iddforce Makandara, aliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wote kwa pamoja
walimuua, Mugisa kwa kumpiga kitu kizito kichwani na kisha kumshambulia kwa
mapanga hadi kufa.Aliiambia mahakama hiyo kuwa mwaka 2005 watuhumiwa hao
walikula njama za kumuua Mugisa ambaye ni mume wake na Catherine John.
Alidai kuwa walifanya hivyo ili
mjane wa marehemu aolewe na Makomelo, huku Lutonja akilipwa sh. 20,000 ili
amsaidie kufanikisha mauaji hayo.Makandara aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu
kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wanaojichukulia sheria
mkononi
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment