WAUGUZI nchini
wameaswa kutotumia migomo kama silaha yao ya kudai maslahi kutoka serikali
badala yake watumie mazungumzo kupitia chama chao.
Hayo yameelezwa na
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Hussein Mwinyi katika Hotuba yake
iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Tabora,Bw.Suleiman Kumchaya katika ufunguzi wa
mkutano Mkuu wa wauguzi Nchini,TANNA,unaofanyika mjini Tabora.
Amesema serikali
inatambua kazi nzuri inayofanywa na wauguzi Nchini na kuwasihi waendelee kutoa
huduma bora kwa wagonjwa wakati Serikali ikiendelea kushughulikia maslahi yao.
Dk.Mwinyi
amewahakikishia wauguzi Nchini kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha wataanza kupewa
posho ya shilingi laki tatu kwa kila mtumishi kwa ajili ya sare kila mwaka.
Awali Mganga mkuu wa
Mkoa wa Tabora,Dk.Leslie Mhina amesema endapo matatizo ya wauguzi yakitatuliwa
ina maana kuwa zaidi ya asilimia sabini ya matatizo katika sekta ya Afya
yatakuwa yametatuliwa.
katika Risala yao
wauguzi wameitaka serikali pamoja na mambo mengi kuwapatia mikopo ya nyumba na
vyombo vya usafiri pasipo riba,wakitaka kulipwa ya kama madaktari wanapoitwa
kufanya kazi kwa dharula na kuwa na kurugenzi ya uuguzi na sio kitengo.
Mkutano huo wa siku
tatu unahudhuriwa na wauguzi zaidi ya elfu moja kutoka Mikoa yote Tanzania bara
huku kauli mbiu yao ikiwa ni kuziba pengo kufikia malengo ya Milenia.
0 comments:
Post a Comment