SERIKALI Mkoani Tabora
itawachukulia hatua wananchi waliojenga juu ya miundombinu ya maji kama mabomba
ili kuepusha hasara kwa wananchi wengi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora,Bi Fatma Mwassa,katika hotuba yake iliyosomwa na mkuuwa
wilaya ya Tabora,Bw.Suleiman kumchaya,wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya
mamlaka ya majisafi na taka,TUWASA,Manispaa ya Tabora..
Amesema itakuwa ni jambo la
ajabu endapo watu waliojenga juu ya mabomba kuachwa pasipo kuchukuliwa hataa
zozote kwani wanahatarisha upatikanaji wa maji kwa walio wengi.
Akizungumzia watu waofanya
uharibifu kwenye vyanzo vya maji,Mkuu wa mkoa amesema nao watashughulikiwa kwa
vile wanahatarisha upatikanaji wa maji ambao ni uhai wa wananchi.
Amesema ni lazima vyanzo vya
maji vilindwe kwa kuhakikisha vinakuwa salama ili wananchi wasitishiwe uhai wao
kwa kukosa huduma ya maji ambayo ni muhimu kwa uhai wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
Bodi ya TUWASA iliyomaliza muda wake,Mchungaji mstaafu Paulo Misigalo,amesema
bodi yake imefanya kazi nzuri ikiwemo kuongeza mapato ya Mamlaka kutoka
shilingi milioni 150 hadi shilingi milioni 230 kwa mwezi na kuifanya mamlaka
kupata hati safi toka Mdhibiti na mkagzui mkuu wa serikali,CAG.
0 comments:
Post a Comment