Home »
» ZIARA YA ZITTO KABWE KANDA YA MAGHARIBI,JIMBO LA IGALULA
ZIARA YA ZITTO KABWE KANDA YA MAGHARIBI,JIMBO LA IGALULA
Siku
ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la
Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya
Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.
Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji
kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao
la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato
wa kuandika katiba.
Kimsingi
shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo.
Hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya
mazao yao na jasho la kazi zao.
Nilipofika
Kijiji cha Loya nimeona eneo kubwa lina miti ya mihama. Wananchi
wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya
yanaharibika tu. Lazima matunda haya yana matumizi yake ya kiviwanda
maana ‘kernel’ yake ina mafuta. Na hili ni swali aliloacha Mh Zitto
Kabwe Nani anajua matumizi ya Mihama?
0 comments:
Post a Comment