BARAZA
la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora jana
limeshindwa kufikia maamzi ya matumizi ya pesa za ushuru wa huduma
Bil 2.3 kutoka mgodi wa dhahabu wa resolute kutokana na baraza hilo
kuvutana dhidi ya matumizi hayo.
Akisoma
taarifa ya kamati ya mipango na fedha Makamu mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo pelle Izengo amesema kuwa kamati hiyo imependekeza
fedha hizo Bil.2.3 zigawanywe kwa kata 37 za halmashauri hiyo
iliziweze kufanya kazi ya ukarabati majengo pamoja na
miundombinu mbalimbali katika kata husika.
Mapendekezo
hayo baadhi ya madiwani wameyapokea kikamilifu na kuunga mkono hoja
hiyo ya ukarabati wa majengo,kuibua miradi ikiwa na kuimalisha
miundombinu mbalimbali huku lengo kuu likiwa ni kuimalisha maendeleo
ya Halmashauri hiyo na wananchi wake.
Karoli
Masanja Diwani wa kata ya Ijanija amesema kuwa fedha hizo zinunue
mashine ya kuchimba visima virefu,Kununua mitambo ya kukarabati
barabara (greda) pamoja na kuanzisha benki ya kijamii itakayo kopesha
wananchi na kukuza uchumi.
Amesema
kuwa mambo hayo yakizingatiwa na Baraza hilo yataweza kukuza pato la
Halmahsuri hiyo na kuongeza ajira kwa wananchi ikiwana kuondoa tatizo
la miundombinu.
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Patrick Mbozu amesema kuwa suala hilo lisubili
wabunge wote wawili Mbunge wa jimbo la Nzega Hamisi kigwangalla
pamoja na mbunge wa jimbo la Bukene Selleman zeddy ili washirikiane
kutoa maamuzi katika baraza maluum.
Akifunga
kikao hicho Mwenyekiti huyo alisema kuwa madiwani wanapaswa kuwa na
changamoto huku lengo kuu likiwa ni moja la kuhakikisha wananchi
wanapata maendeleo na kutatua kero zao.
1 comments:
MI NAONA HIZO PESA ZITUMIKE KUMALIZIA BARABARA YA BUKENE KWENDA SEMEMBELA KWANI NI KIPANDE KIDOGO KILICHOBAKI KUFIKA SEMEMBELA PIA KUNA KALAVATI MOJA PALE KAGANDO AMBALO LILISOMBWA NA MAJI PESA HIZO ZIFANYE KAZI PALE
Post a Comment