Home » » BIL 2.3 ZA MGODI ZAWAGAWA MADIWANI NZEGA

BIL 2.3 ZA MGODI ZAWAGAWA MADIWANI NZEGA

BARAZA la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora jana limeshindwa kufikia maamzi ya matumizi ya pesa za ushuru wa huduma Bil 2.3 kutoka mgodi wa dhahabu wa resolute kutokana na baraza hilo kuvutana dhidi ya matumizi hayo.
Akisoma taarifa ya kamati ya mipango na fedha Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pelle Izengo amesema kuwa kamati hiyo imependekeza fedha hizo Bil.2.3 zigawanywe kwa kata 37 za halmashauri hiyo  iliziweze kufanya kazi ya ukarabati majengo pamoja na miundombinu mbalimbali katika kata husika.

Mapendekezo hayo baadhi ya madiwani wameyapokea kikamilifu na kuunga mkono hoja hiyo ya ukarabati wa majengo,kuibua miradi ikiwa na kuimalisha miundombinu mbalimbali huku lengo kuu likiwa ni kuimalisha maendeleo ya Halmashauri hiyo na wananchi wake.

Karoli Masanja Diwani wa kata ya Ijanija amesema kuwa fedha hizo zinunue mashine ya kuchimba visima virefu,Kununua mitambo ya kukarabati barabara (greda) pamoja na kuanzisha benki ya kijamii itakayo kopesha wananchi na kukuza uchumi.

Amesema kuwa mambo hayo yakizingatiwa na Baraza hilo yataweza kukuza pato la Halmahsuri hiyo na kuongeza ajira kwa wananchi ikiwana kuondoa tatizo la miundombinu.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Patrick Mbozu amesema kuwa suala hilo lisubili wabunge wote wawili Mbunge wa jimbo la Nzega Hamisi kigwangalla pamoja na mbunge wa jimbo la Bukene Selleman zeddy ili washirikiane kutoa maamuzi katika baraza maluum.

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti huyo alisema kuwa madiwani wanapaswa kuwa na changamoto huku lengo kuu likiwa ni moja la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kutatua kero zao.

1 comments:

WILLIAM MANDI said...

MI NAONA HIZO PESA ZITUMIKE KUMALIZIA BARABARA YA BUKENE KWENDA SEMEMBELA KWANI NI KIPANDE KIDOGO KILICHOBAKI KUFIKA SEMEMBELA PIA KUNA KALAVATI MOJA PALE KAGANDO AMBALO LILISOMBWA NA MAJI PESA HIZO ZIFANYE KAZI PALE

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa