Home » » HOT NEWS: JWTZ,Polisi na wale wa hifadhi kwenye kashfa ya mauaji ya raia Tabora‏

HOT NEWS: JWTZ,Polisi na wale wa hifadhi kwenye kashfa ya mauaji ya raia Tabora‏

Marehemu enzi za uhai wake kabla hajakutwa na
mauti,akidaiwa ni jambzi,mhamiaji haramu na anamiliki silaha licha ya
kutopatikana silaha yoyote.
Mama mzazi wa marehemu Magerth Kajoro Kashimba akitoa maelezo kwa mwandishi wa makala hii jinsi mtoto wake alivyouawa.




Hali halisi ya picha zinzvyoonyesha jinsiaskari hao wa JWTZ,Polisi na wale wa wanyama pori walivyochana chana magodoro,kuvunja vitanda na kumwaga mahindi chini kabla hawajatesa na kuua raia.

Na mwandishi wetu-Tabora yetu
ILIKUWA ni siku ya jumapili majira ya saa tisa alasiri wakati askari
wa JWTZ, askari Polisi na wale wa maliasili walipofika nyumbani na
kumtaka mtoto wangu Kipala Issa (39) wakimtuhumu anamiliki silaha bila
kibali na pia ni mhamiaji haramu na jambazi.

Ujio wa askari hao hadi sasa umeniachia simanzi kwani mtoto wangu
Kipala Issa alipoteza maisha akiwa nchini ya ulinzi wa askari hao
baada ya kuteswa na kupigwa sana akitakiwa aonyeshe silaha aina ya
SMG.

Hayo ni maneno ya mama wa marehemu Magreth Kajoro Kashimba (53) wakati
akisimulia mkasa huo nyumbani kwa marehemu mwanaye siku ya jumatano
kijiji cha Usinnge wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Kashimba anasema siku ya jumapili majira ya saa tisa alasili alikuwa
akitoka kanisani ghafla aliliona gari la jeshi la JWTZ likipita kwa
kasi kuelekea nyumbani kwa marehemu mwanaye.

Anasema baada ya kufika nyumbani alikuta gari hilo likiwa limepaki nje
ya nyumba huku askari wa JWTZ nje wako nane na ndani wapo wanne.

“Niliopingia nadani nilikuta askari watatu wapo sebuleni na mmoja yupo
stoo ya vyombo nilipigwa na mshangao hawa wanataka nini.”alisema.

Alisema wanilinuliza wewe ndiye mama wa nyumba hii ni aliwajibu yeye
ni mama wa mtoto mwenye nyumba hiyo.

Aidha askari hao walimuuliza tena milango fremu zaidi 128 ya nani
aliwajibu ya mtoto wake Kipala Issa.

Alisema walimuulizia Kipala mwenyewe yuko wapi na aliwajibu yupo shamba.
“Waliuliza tena tunasikia mtoto wako anamiliki silaha aina ya SMG na
kombati za jeshi…..niliwaleza sijawahi kumuona na kombati za jeshi
wala silaha hiyo na mtoto wangu hana tabia ya ujambazi.”alisema.

Alisema walimueleza ampigie mtoto wake ili aje wana shida naye na
ndipo mrehemu Issa alipopata taarifa na kupiga simu akahoji kuna nini
ndipo alipoambiwa na mama yake kuna wanajeshi wanashida naye akasema
anakuja.

“Wakati hayo yakiendelea askari mmoja aliniuliza kama nimshawahi
kusikia na kutamkia kuwa siyo wote walio geezani wana makosa.”alisema.

Kashimba alisema askari hao waliondoka na kuahidi wakirejea wamkute
mtuhumiwa huyo au wapelekwe anapolimia lakini walielezwa ni mbali ila
atakuja tu.

Alisema baada ya dakika tano hivi mama huyo alisema zilikuja gari tatu
moja ubavuni imeandikwa OCD Tabora,moja ya jeshi JWTZ na mbili
yaaskari wa maliasili.

Alisema baada ya kurejea waliingia ndani na kukuta vijana wa shule ya
sekondari ya kata ya Usinge wakijisomea na vijana wale waliamrishwa
wabebe fremu za milango 128 wapakie kwenye gari.

“Walichukua fremu za milango 128,pikipiki mbili aina ya SALG yenye
namba za usajili T 765 BWL  T 535 AWT aina ya Baja ,mbao 80,simu mbili
moja ya marehemu na nyingine ya kijana mmoja wa sekondari. Na vitu
hivyo walikuwa wakivipeleka ofisi za maliasili”alisema.

Kashimba aliongeza baada ya kuchukua vitu hivyo walianza kuwaambia
wale vijana wanafunzi wabebe mahindi gunia 150 za mahindi,gunia 2 za
maharage na gunia 3 za mpunga wazitoe nje.

Anasema walichana magunia yale na kuanza kumwaga mahindi wakichanganya
na maharage na mpunga huku wale wanafunzi wanaobeba gunia hizo wakidai
wamechoka walikuwa wakipigwa viboko.

Aliongeza baada ya hapo walimuita mke wa marehemu ambaye ni askari
mwenye namba inahifadhiwa,aliyejulikana kwa jina la WP Tabu na
kuamriwa afungue chumba wanapolala.

Hata hivyo wakati mke wa marehemu anafuata funguo askari hao walivunja
mlango kwa mateke na kuingia ndani wakaanza kuchana nguo,wakapekua na
kwa mujibu wa mke wa marehemu PC Tabu ndani kulikuwa n ash milioni
zaidi ya 25.

Mama wa marehemu huyo anaongeza baada ya kutoka chumbani walimuita
mdogo wa marehemu Hassan Issa Mohamed (28),mke wa marehemu PC Tabu na
mama wa marehemu Magreth Kashimba na wakawa wanawapiga kwa makofi
mateke na mpini wa jembe huku wakiwaelekezea bunduki vichwani
kuwaamuru waonyeshe silaha.

“Walinieleza wanachotaka ni silaha na wakauliza bunduki ipo au na
wakanitaka nipige goti nisali  sala ya mwisho…..lakini niliwaeleza leo
ni siku ya jumapili nimeshapiga goti kusali kwa Mungu wangu.”alisema.

Alisema nilipigwa na mpini wa jembe mkononi mara tatu nikapoteza
fahamu lakini mashuhuda waliokuwepo walisema niliendelea kupigwa tu
pamoja na kupoteza fahamu.

Anasema wakati anazinduka alimuita mke wa marehemu mtoto wake PC Tabu
naye anasubulubiwa vikali kwa mateke na fimbo huku akimwagiwa maji
zaidi ya ndoo tano wakimtamkia askari mzima unaolewa na jambazi sasa
leo ndiyo mwisho wao.

Aidha Kashimba anasema wakati hayo yakiendelea mdogo wa marehemu
mwingine ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Anthony Erickzanda
Gaberiel (18) naye alipigwa na kuchomwa kisu ubavuni na kuzimia baada
kumwaga damu.

Anafafanua kuwa baada ya mateso ya muda mrefu ndipo marehemu Kipala
Issa alipofika na askari hao walipomuona walipiga risasi moja juu naye
alinyanyua mikono juu kusalimu amri.

Aliulizwa huyo ni ani yako marehemu Kipala alijibu ni mke wangu na
kuulizwa tena bunduki unayomiliki iko wapi na alichukuliwa hadi ndani
ambapo ndani ya dakika tan walimtoa nje akiwa anavija damu mdomoni na
puani akiwa na pingu mikononi.

“Walimchukua mtoto wangu wakaondoka naye kwenye magari hatukujua
wanampeleka wapi. licha kuiokosa bunduki waliyokuwa wakiitafuta
”alisema.
Siku ya jumatatu

Kashimba anaongeza siku ya jumatatu mdogo wa marehemu Rifat Dickson
Mboya  na mke wa marehemu PC Tabu kwenda kaliua kumtafuta Kipala Issa
bila mafanikio.

Aidha alisema walipata taarifa kuwa Kipala Issa amefariki kwa kipigo
na mwili wake ulipelekwa mochwari Tabora na kukataliwa ukarejeshwa
mochwari ya hospitali ya wilaya ya Urambo mwili huo ukahifadhiwa.

Anasema walirejea hadi hospitali ya wilaya ya Urambo na walipopelekwa
mochwari ndipo waliukuta mwili wa marehemu baada ya kuutambua.

Mama wa marehemu anasema awali walitakiwa wachukue mwili lakini
waliikataa maiti hiyo kwani hakukuwa na uchunguzi uliofanywa dhidi ya
marehemu kuwa alikufa kwa kipigo ama la.

Anasema siku ya jumatatu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Peter Ouma
na kamanda wa polisi wilaya ya Kaliua OCD Mnubi walifika eneo la tukio
na kuelezwa kila kitu na ndipo RPC amamueleza OCD afungue “kesi ya
mauaji” ambayo ina namba KAU/IR/1216/2013 na hadi sasa uchunguzi
unafanyika.

Mkuu wa mkoa Tabora anena na wafiwa.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa alifika kijiji cha Usinge siku ya
alhamis ya mwezi oktoba 17,mwaka huu na alizungumza na wafiwa,mke wa
marehemu na ndugu na kuwahaahidi tukio hilo litafanyiwa uchunguzi.

Hata hivyo mkuu wa mkoa aliwataka wananchi wa kijiji cha Usinge
kuwafichua wahamiaji haramu na watu wanaomiliki silaha,na alikiri
kuumizwa sana mauaji na hayo na kuhaidi kulitafutia ufumbuzi wa
haraka.

Hadi sasa hauna askari yoyote aliyekamatwa kwa tukio hilo na mwili wa
marehemu ulizikwa siku ya jumatano kijijini Usinge mahali alipozaliwa
licha kuwa ni muha wa mkoa wa Kigoma.

Kashimba anasema marehemu mtoto wake ameacha mke na watoto wanne
Zinedine Kipara (12),Regina Kipara miezi mitano,David Kipara
(9),Johnson Kipara (6),



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa