Home » » VIONGOZI 9 TABORA KUFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI KESHO

VIONGOZI 9 TABORA KUFIKISHWA MBELE YA BARAZA LA MAADILI KESHO

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma inawafikisha viongozi wa umma 9 mbele ya baraza la maadili kwa tuhuma mbalimbali za ukiukwaji maadili ya uongozi. Kwa mujibu wa taarifa ilioyotolewa na Afisa habari wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Bw. Kajiru Shabani, imesema baraza hilo litaketi 13 hadi 22 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mjini Tabora. Afisa habari huyo amesema miongoni mwa makosa wanayotuhumiwa nayo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kutoa tamko la rasilimali na madeni na kutoa tamko la uongo ikiwa ni kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 15 vya sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 15 ya mwaka 1995 kifungu 15(a ). Bw. Shabani amesema hatua hizo za kinidhamu zimeainishwa katika kifungu cha 8 cha sheria ya maadili, ikiwa ni pamoja na kuonywa, kupewa tahadhari, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi, kufukuzwa kazi na kushauriwa kujiudhuru wadhifa husika sanjari na kupewa adhabu nyigine kwa mujibu wa sheria ya wadhifa wake. Aidha baraza hilo linaundwa na sheria ya maadili chini ya kifungu cha 26 kwa sasa Mwenyekiti wake ni Mhe. Barozi Jaji Hamisi Msumi wajumbe wa kiwa ni bibi Celina Wambura na Bibi Hilda Gongwe, baraza hilo leo litaketi kwa mara ya tatu toka kuanzishwa kwake. Baraza la maadili lina majukumu ya kupokea malalamiko kutoka kwa kamishina wa maadili Nchini na kufanya uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kumshauri Rias wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi wa umma.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa