BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora
limeomba kuidhinishiwa kiasi cha sh 35,455,837,199 kwa mwaka wa fedha
wa 2014/2015.
Akisoma taarifa ya bajeti hiyo, Kaimu Ofisa Mipango wa halmashauri
hiyo, Martin Jakanyango, alisema kiasi hicho kinajumuisha sh
1,378,203,500 kama vyanzo vya ndani vya halmashauri.
Jakanyango alitaja kuwa ruzuku ya fidia ya kodi waliyopanga ni sh
579,594,000, ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya mishahara ni sh
23,978,711,716.
Alitaja ruzuku kwa ajili ya matumizi ya kawaida ni sh 2,911,348,000,
ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni sh 5,326,293,982, ruzuku kwa
ajili ya mifuko ya pamoja ni sh 1,231,686,001 huku michango ya
wahisani ikiwa sh 50,000,000.
Katika kikao hicho, baraza hilo lilipitisha bajeti ya halmashauri ya
mji mdogo wa Nzega kiasi cha sh 1,012,372,763 kwa mwaka huo wa fedha.
“Taarifa hiyo inasema kiasi cha sh 1,228,220,000 kitatokana na vyanzo
vya ndani, fidia ya kodi sh 360,000,000 na ruzuku kutoka Serikali Kuu
sh 807,526,190,” alisema.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment