Na Hastin Liumba,Igunga
SERIKALI ya wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora imefanikiwa kuhamasisha
jumla ya vitongoji 624 kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibarik Kingu alisema hayo katika kikao cha
wadau wa mfuko wa afya ya jamii tiba kwa kadi (TIKA) kilichofanyika
mkoani Tabora.
Alisema licha ya kuvifikia vitongoji hivyo pia wamepania kufikisha
idadi ya wanachama wanaopata huduma ya mfuko huo 20,000 ifikapo mwaka
2014.
Kingu aliongeza kuwa kufikia malengo bado kunahitaji watendaji
waadilifu na kwamba Igunga imefanikiwa kwenye huduma za afya hasa
kutokana na kuwepo watendaji wanaojituma na waadilifu.
“Watendaji sisi tunapaswa kubadilika…..tatizo tumekuwa tukikiongea
sana,siasa na kufanya kazi kwa mazoea tukubali kubadilika.”aliongeza.
Alisema ifikie mahali sasa viongozi wa chi yetu tuwe wa mfano na
kuongoza wananchi wetu.
Aidha aliwataka viongozi wa Tabora manispaa kuacha tabia ya kukomoana
na badala yake wanapaswa kumtumia mkurugenzi wa sasa Alfred Luanda ili
mji wa Tabora ufanikiwe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa Tabora Alfred Luanda ambaye
mfuko wa Taifa wa bima ya Ayfa ulikuwa ukizindua na kupitisha sheria
ya huduma ya tiba kwa kadi TIKA katika manispaa Tabora,alisema
amefarijika sana huduma hiyo kuanzishwa.
Luanda alisema ili kufanikiwa ameomba watendaji kuacha tabia ya
kufanya kazi kwa kukomoana,majungu na fitna.
Alisema kazi waliyopewa ni ya wananchi hivyo kuwepo visasi,majungu na
kukatishana tamaa hakutaisadia manispaa Tabora.
Alitaka watendaji kuchukua hatua za kiutendaji na siyo kufanya kazi
kwa faida ya kiongozi fulani kwani ni hatari.
Home »
» IGUNGA YAHAMASISHA VITONGOJI 624 KUJIUNGA CHF.
0 comments:
Post a Comment