Na Hastin Liumba,Sikonge
- Ni chama cha wakulima 700 wa zao la tumbaku.
- chama kinalipia watumishi wake makato ya NSSF.
- Msimu huu wa 2013/2014 walenga kuzalisha kilo 1,400,000 za thamani ya sh bilioni 6.2.
CHAMA cha msingi Kisanga, kilichopo wilaya ya
Sikonge mkoani Tabora,ni chama cha wakulima wa zao la Tumbaku ambacho kimekuwa
kikijiendesha kwa mafanikio hadi sasa toka kimeanzishwa.
Chama hiki kilianzishwa mwaka 1998 kikiwa na
wanachama 120 chenye namba za usajili za la Kisanga Amcos Ltd kimepewa usajili
namba 540-TBR, hadi sasa chama kina wanachama 700.
Rashid Mazinge ni mwenyekiti wa chama cha msingi
Kisanga na hapa anaelezea historia ya chama hicho kwa mwandishi wa habari wa
makala hii toka kimeanzishwa mwaka 1998 kikiwa na wanachama 120 tu.
Mazinge anasema chini ya uongozi wake chama
alikikuta kikiwa na wanachama 250 na kutokana na kusimama imara katika kutetea
maslahi ya wakulima wanachama wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku.
Anaongeza kuwa hadi kufikia msimu wa kilimo mwaka
2012/2013 chama kilikuwa na wanachama 600 na kupokea wanachama wapya 100 msimu
wa 2013/2014 na kufikisha wanachama 700 hadi sasa na wamefanikiwa kupata faida
kila msimu wa kilimo kila mwaka.
Mazinge anaelezea mikakati, malengo, faida na changamoto
chache kwa chama hicho na kusema asilimia kubwa ya shughuli za kilimo chao ni
faida kutokana na kujipanga vyema katika kilimo.
Uzalishaji
msimu wa 2012/2013
Anabainisha
Chama kilikopa mkopo wa pembejeo Benki ya NMB Dola 692,000 sawa na sh 411,740,000 na
Chama kilinunua pembejeo na kuwakopesha wanachama kwa jitihada ya wanachama,
walizalisha kilogramu za tumbaku 940,049 zenye thamani ya dola 1,846,132 ya ni
thamani ya sh 2,935,349,880.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa kipindi cha msimu
wa 2012/2013 hakuna mkulima alilaza deni wala kudai katika chama cha msingi.
Aliongeza kutokana na uzalishaji huo walifanikiwa
kuzalisha tani zenye thamani ya Dola 2,538,132 kiasi ambacho walilipa mkopo
Benki ya NMB tawi la Sikonge na kubakiwa na kiasi cha Dola 1,846,132 Sawa na
Tshs 2.935,349,880 kiasi ambacho kililipa wakulima kwa asilimia 100.
Aidha alisema kuwa kwa uzalishaji huo chama kimepata
ushuru wa Dola 65,805 sawa na Tsh.104,629,950.
Mwenyekiti huyo alisema msimu huo hakukuwa na
matatizo kutokana na wakulima wote walilipwa fedha zao,hakukuwa na utoroshaji
wa tumbaku.
Changamoto
kwa msimu wa 2012/2013.
Mazinge alisema kutokana na changamoto ya ukosefu wa
maghala ya kuhifadhia tumbaku wanachama waliazimia kujenga ghala na hadi sasa
wamechangia Dola 31,000 sawa na sh.49,290,000 ambapo Chama kimechangia Dola
ya10,000 sawa na pesa ya Kitanzania 15,900,000.
Aidha alisema ghala wanalotarajia kujenga
linakadiriwa kutumia kiasi cha sh ujenzi wa ghala hilo unatarajia kugharimu
kiasi cha sh 99,000,000 ghala ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua tani 10 hali
ambayo itasaidia kuondoa changamoto hiyo.
Alisema wakulima walikuwa wapata shida ya kuokosa maghala
kwani walilazimika kukodo maghala vijiji vya jirani katika kata ya Mole, Kisanga,Mwamayunga
na Utyatya ili kuhifadhia tumbaku yao kipindi cha masoko.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa chama pia kimepitisha
matumizi ya sh 19,000,000 kama posho ya mkutano mkuu wa wanachama mwezi
februari 15,2014 msimu huu wa kilimo wa 2013/2014.
Michango
ya maendeleo.
Mazinge alisema kutokana na umuhimu wa kutambua
maendeleo ya kata hiyo chama kupitia wanachama wake wametoa kiasi cha sh
3,000,000,000 zitumike kwenye ujenzi wa ofisi ya kata ambayo tayari ujenzi wake
umeshaanza.
Kutokana
na changamoto za mikopo.
Aidha mwenyekiti huyo alisema kutokana na changamoto
nyingi za mikopo chama kimeamua kuanzisha SACCOS inayojulikana kwa jina la
Kisanga Saccos.
Aliongeza kuwa Chama kimeanzisha mfuko wa pembejeo SACCOS
wanachama wamechangia Dola 21,000.sawa na Tsh 33,390,000 kutokana usumbufu
wanaopata pindi wanapokwenda kukopa katika taasisi za fedha na kiasi hicho kipo
benki.
Alisema kila mwanachama katika chama hicho ametakiwa
kuchangia kiasi cha dola 65.
Aidha alibainisha kuwa SACCOS hiyo itaanza
kukopeshana pale wataalamu toka ofisi ya mkurgenzi wa halmashauri idara ya
ushirika watakapokwenda kutoa muongozo.
Kwa uzalishaji wao mzuri wanachama waliamua kujilipa
posho kila mmoja Tsh.15,000 sawa na 9,000,000 kwa wanachama 600.
MSIMU
2013-2014.
Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa Chama kimekisia
Mkopo wa pembejeo Dola 968,000 sawa ns sh 1,539,120,000 kutoka Benki ya NMB,ambapo
chama kimekisia kupata kilogramu za tumbaku 1,400,000 zenye thamani ya dola
3,920,000 sawa na thamani ya sh 6,272,000,000 .
Aidha mwenyekiti huyo alisema kutokana na mkopo huo
wanachama wameendelea kupokea pembejeo zao kulingana na mahitaji yao.
Aidha alifafanua kuwa katika suala la uzalishaji
chama kimekisia mauzo ya Dola 3,920,000 sawa na Tsh 6, 272,000,000 ambayo italipa
mkopo wa Benki na kubakiwa na Dola 2,952,000 sawa na Tsh 4,723,200,000.
Alisema fedha hizo zitalipwa na wakulima kwa
Asilimia 100 na Chama kimekisia kupata ushuru Dola 98,000 sawa na Tsh 156,
800,000.
Changamoto
za msimu wa 2013-2014.
Alisema ili kuuendeleza mfuko wa pembejeo kwa
wanachama SACCO, wanachama wanategemea kuchangia Dola 84,000 sawa na
Tsh.134,400,000.
Mazinge alisema mfuko huo wa pembejeo kwa msimu wa
2013/2014 chama kitachangia Dola 10.000 sawa na Tsh 16,000,000 kwa maana mfuko
huo wa pembejeo utakuwa na Thamani ya Dola 115,000.sawa na Tsh 184,000,000.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kulingana na kupanuka
kwa chama, chama kimeamua kununua Computer
yenye thamani ya Tsh 5.200,000 kwa msimu huu 2013/2014.
Aidha alisema wanachama pia waliazimia ununuzi wa
gari aina ya fuso lenye thamani ya Tsh.30,000,000 kwa ajili ya kusafirisha
pembeje na tumbaku ya wakulima.
Aidha alisema wanachama kwa kauli moja wamekubaliana
kupitisha kiasi cha 10,500,000 kwa ajili ya posho na mkutano mkuu wa chama kwa
msimu wa 2014/2015.
Aliongeza kuwa chama kimetenga pia kiasi cha sh 2,000,000
za ununuzi wa viti 100 kwa ajili ya wanachama kwenye mikutano yao na kutenga
kiasi cha sh 570,000 kwa ajili ya malipo kwa ajili ya NSSF kwa watumishi wa
chama chao.
Changamoto
kuu.
Mazinge alibainisha changamoto kuu kwao kwa sasa
kuwa ni mikopo ya pembejeo ikiwemo kuchelewa kwani pembejeo hiyo inakuja bila
kuendana na kalenda ya kilimo.
Alitaja changamoto nyingine ni ukosefu wa
miundombinu ya barabara kwani kumekuwa na ugumu sana kwenye usafirishaji wa
tumbaku na pembejeo kwani hali ya barabara zao toka makao makuu ya wilaya ya
Sikonge kuja kwenye kata siyo nzuri.
Aidha changamoto nyingine ni ukosefu wa maji safi na
salama kwani maji watumiayo ni ya visima na madimbwi,miundombinu ya umeme kwani
wananchi wana muamkom wa uchangiaji umeme.
Mwenyekiti
wa kijiji cha kisanga anena.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kisanga Yasin Matandula
alitoa wito kwa jeshi la polisi kuangalia kwa umakini suala la usalama katika
kata ya Kisanga kwani ni kata inayozalisha fedha nyingi sana za tumbaku.
Chama cha msingi Kisanga kinaundwa na mwenyekiti
Rashid Mazinge,Waziri Mwilia makamu mwenyekiti,Seleman Msumeno,Ali
Shaban,Mohammed Mwinyi,Issa Maliki,Yusuph Matandula,Nathan Peter na Athuman
Majaliwa na diwani wa kata hiyo ni Abdalalh Msumeno na katibu meneja ni Athuman
Malela.
0 comments:
Post a Comment