Home »
» Majambazi wateka magari, wafanya ukatili wa kutisha
Majambazi wateka magari, wafanya ukatili wa kutisha
WATU
wanaodhaniwa kuwa majambazi, usiku wa kuamkia jana wameteka magari
mawili ya mafuta na kuwadhuru watu waliokuwa kwenye magari hayo kwa
kuwakata mapanga na wengine wakidaiwa kukatwa masikio.
Tukio hilo lilitokea katikati ya Kijiji cha Kitangili na Miguwa nje kidogo ya Mji wa Nzega, mkoani Tabora.
Inadaiwa kuwa, magari hayo yalikuwa yakitokea nchini Burundi kwenda Dar es Salaam ambapo watekaji hao walikuwa wakitaka fedha.
"Walipoambiwa
fedha hakuna, hawa majambazi walisisitiza fedha wanazo kwani wametoka
safari ya mbali hivyo wasipotoa watawadhuru, walianza kuwapiga kwa
mapanga na kuwajeruhi.
"Tukio hili halikuwafurahisha wakazi wa Nzega
na madereva wengine wa magari ya mizigo hivyo wamefunga barabara
wakishinikiza kutaka waonane na Mkuu wa Mkoa Bi.Fatma Mwassa, wamueleze
kilio chao," alisema mkazi wa eneo hilo katika eneo la tukio.
Madereva
wa magari makubwa waliozungumza na Majira, walisema eneo hilo limekuwa
likitumika kama kichaka cha kutekea magari na kujeruhi wananchi.
Kwa
upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Dkt. Emmanuel Mihayo,
alisema amepokea majeruhi watatu usiku wa kuamkia jana wakiwa
wamejeruhiwa vibaya.
Alisema mmoja kati ya majeruhi hao alikuwa
hajitambui na wengine wawili wakiwa mmoja kati yao amekatwa sikio na
shavu la kushoto kwa mapanga na mwingine mguu.
Dkt. Mihayo alisema, bado wanaendelea na matibabu kwa majeruhi wote ambao hakuwataja majina yao
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment