Home » » MSINGI WA MAENDELEO NI AMANI-NTAHONDI.

MSINGI WA MAENDELEO NI AMANI-NTAHONDI.

Na Hastin Liumba,Uyui

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Tabora (Uyui) Said Ntahondi, amesema msingi mkubwa wa maendeleo eneo lolote lile ni amani.
Ntahondi alisema hayo wakati alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Utula kata ya Mabama wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Alisema amani tuliyonayo tunapaswa kujivunia na kwamba amani hiyo inatakiwa kuanzia ngazi ya Kaya,Kitongoji,Kijiji hadi Kata.
“Kama amani hakuna eneo lolote lile maendeleo yake kupatikana ni ndoto kwani wakati wote jamii huishi kwa hofu kubwa.”aliongeza.
Alisema wananchi wanatakiwa kupima ule mwafaka wa vyama vya CCM na CUF kule Zanzibar hiyo yote ni vigezo vya amani tuliyonayo watanzania.
Alisema serikali za awamu zote zinapaswa kupongezwa kwa kuisimaia amani tuliyonayo kiasi kupiga hatua ya maendeleo leo hii.
Hata hivyo Ntahondi alisema amani tuliyonayo haitakuwa na maana endapo wananchi hatutafanya kazi kwa bidii,kujua haki zetu na kuheshimu sheria tulizojiwekea
Alisema amani hii pia imesadia kukuza uchumi wa nchi kwani uchumi wa mwaka 1961 siyo mwaka 2014 sasa hivyo tuna kila sababu ya kujipongeza
Alisema uchumi wowote ule unaokuwa hauwezi kukua kwa kupiga kelele vijiweni na badala yake tunapaswa kuchapa kazi kwa bidiii.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa