CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kitaendelea kutimua
wasaliti na kutaka wananchi kuendelea kuwaunga mkono kwenye
operesheni maalumu ya M4C Pamoja Daima.
operesheni maalumu ya M4C Pamoja Daima.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alisema hayo kwenye viwanja vya Shule
ya Sekondari Uyui wakati akiongea na wananchi kwenye mkutano wa
hadhara.
hadhara.
Mnyika alisema hayo baada ya awali kukaribisha maswali ya wananchi
ambao karibu wote waliopata nafasi ya kuuliza walilenga kutaka kujua ni
vipi suala la Zitto Kabwe litamalizwa.
Akijibu maswali hayo Mnyika alisema CHADEMA inaendesha mambo yake kwa
kuzingatia kanuni, taratibu na sheria, hivyo suala la Zitto
lilishamalizwa, lakini chama kitaendelea kutimua wasaliti wote.
”Ndani ya CHADEMA hakuna kulindana kama CCM wanavyofanya, na madhara yake leo tunayaona nchi inashindwa kupiga hatua.
”CCM wamekuwa wakilindana na ndiyo maana hawana utaratibu wa
kuwajibishana… sisi hatuna hiyo stahili, tutaendelea kuchukua hatua,”
alisema Mnyika.
Alitolea mfano mwaka 2009 usaliti ndani ya chama ulianza kwa baadhi
ya viongozi, pia mwaka 2010 baadhi ya viongozi walisaidia viongozi wa
CCM kushinda uchaguzi wa majimbo.
Alisema maadui wa CHADEMA kisiasa wamekuwa wakipandikiza mamluki ili
kusaliti nguvu ya CHADEMA, na kwamba suala la chama kutimua viongozi ni
utaratibu wa kikatiba.
Alisema kitendo cha Zitto kukimbilia mahakamani, kwa kanuni za CHADEMA amejivua uanachama mwenyewe na yeye analitambua hilo.
Akijibu swali la vijana kupata elimu hasa katika mikopo, alisema
msimamo wa CHADEMA haukubaliani na mfumo mzima uliopo, ikiwemo bodi
yenyewe ya mikopo.
Alisema suala la elimu ni haki ya vijana, hivyo ni haki na siyo jambo
la kukopeshana licha ya kuwa ni suala la kikatiba Makamu Mwenyekiti wa
CHADEMA taifa, Said Issa Mohammed, aliwataka wananchi kushirikiana,
kushikamana ili kuiangusha CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu na kwamba anachoona katika mikutano
ya CHADEMA, virungu na mabomu yanayopigwa na askari polisi, ni askari
hao kuwashangaa wananchi kuchelewa kuiondoa CCM madarakani.
Aligusia elimu na kushangazwa na watoto wa Kitanzania wanapokwenda
shule hubeba panga na jembe huku wenzetu wa Uganda watoto wa darasa la
pili wanaenda shule na kompyuta za mkononi (Laptop).
Kuhusu chama hicho kuhusishwa na ukanda, Uchaga ama chama cha
kikanda, alisema wanaoeneza ujinga huo wanatakiwa kupimwa akili kwani
kinachoangaliwa ndani ya CHADEMA ni uadilifu na uwezo kwani chama hicho
ni mali ya wananchi na si uongozi.
Makamu mwenyekiti huyo aliongeza kuwa CCM wameandaa mikakati mingi ya kuwadhoofisha kwa kununua baadhi ya viongozi wao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment