Na Hastin Lumba,Sikonge
SIKONGE KUTUMIA SH BILIONI 22.6 MWAKA WA FEDHA 2014/2015
BARAZA la Halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imeomba
kuidhinishiwa kiasi cha sh 22,673,464,095 kwa mwaka wa fedha wa
2014/2015.
Hayo yalipitishwa na baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Sikonge kwenye kikao chao wilayani humo.
Akisoma taaarifa yake ya bajeti afisa mipango wa halmashauri hiyo
Ernest Kahabi alisema katika bajeti hiyo kiasi cha sh 13,837,600.595
ni mishahara na sh 2,532,489,800 ni maumizi mengineyo.
Kahabi aliongeza kuwa kiasi cha sh 3,716,873,700 kitatumika kama
miradi ya maendeleo ambapo fedha za ndani ni sh 1,985,987,900 na fedha
za nje ni sh 1,419,195,800.
Kahabi aliongeza kuwa kiasi cha sh 311,690,000 ni fedha ambazo
zitatoka kwa wahisani shirika lisilo la kiserikali la EGPAF.
Aidha alifafanua kuwa fedha zitokanazo na mapato ya ndani ni sh
2,241,45000 ambapo sh 1,176,500,000 ni kwa matumizi ya kawaida
(mishahara sh 58,000,000 na matumizi mengineyo sh 1,118,500,000).
Kahabi aliongeza kuwa fedha za miradi ya maendeleo sh 1,064,950,000 na
matumizi yanayofanywa kwa kuchangia huduma ni sh 60,000,000 CHF/NHIF
na ada za shule za sekondari sh 126,540,000.
Kahabi alisema vyanzo vya mapato ya ndani vitatokana na ushuru
mbalimbali wa leseni zabiashara,ada za ardhi,kuuza viwanja,maombi ya
viwanda na ushuru nyumba za kulala wageni.
Vingine ni leseni za vileo,ushuru wa vibanda,kodi ya majengo,ushuru wa
tumbaku,ushuru wa pamba,ushuru wa mazao ya chakula,maombi ya
zabuni,ushuru wa machinjio,leseni za mazao ya misitu na ushuru wa
mazao ya nyuki.
Home »
» SIKONGE KUTUMIA SH BILIONI 22.6 MWAKA WA FEDHA 2014/2015
0 comments:
Post a Comment