Home » » Sikonge yapitisha mapendekezo ya Bajeti

Sikonge yapitisha mapendekezo ya Bajeti

BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Sikonge  limeidhinisha mapendekezo ya Bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 22.6 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Akisoma taarifa ya Bajeti hiyo Afisa Mipango wa halmashauri hiyo,Bw. Ernest Kahabi amesema  kiasi cha shilingi Bilioni 13.8  zitatumika kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa kada mbalimbali na shilingi Bilioni 3.7 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kahabi ameongeza kiasi cha shilingi Bilioni 2.5 kimetengwa kwa ajili ya matumizi mengineyo ambapo fedha za ndani  ni shilingi Bilioni 1.9.

Kahabi amesema vyanzo vya mapato ya ndani vitatokana na ushuru mbalimbali wa leseni za biashara, ada za ardhi, kuuza viwanja, maombi ya viwanja na ushuru wa nyumba za kulala wageni.

Vyanzo vingine ni leseni za vileo, ushuru wa vibanda, kodi ya majengo, ushuru wa tumbaku, ushuru wa pamba, ushuru wa mazao ya chakula, maombi ya zabuni, ushuru wa machinjio, leseni za mazao ya misitu na ushuru wa
mazao ya nyuki.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa