Home » » WAKAZI WA IGURUBI WAUKATAA MRADI WA MACHINJIO

WAKAZI WA IGURUBI WAUKATAA MRADI WA MACHINJIO

WAKAZI wa Tarafa ya Igurubi wilaya ya Igunga,wamekataa kupokea mradi wa machinjio kwa madai kuwa haupo katika ubora unaotakiwa kutumika kama machinjio

Wakizungumzia mradi huo,wakazi hao wamesema  umejengwa kwa kuwekewa mabati chakavu pamoja na mbao hali ambayo unaufanya uonekane haukidhi viwango vya ubor.a

Wakiongozwa na Sultan Ahmed na Isaya Lameck, wamesema wakiwa wakazi wa tarafa ya Igurubi wanasikitishwa kuona fedha za Serikali zikifujwa na wachache wasio waaminifu

Afisa Mtendaji wa Kata ya Igurubi,Mdeka Seleman amekiri mradi huo kuwa chini ya kiwango akieleza  kuwa mkandarasi aliyejenga machinjio hayo alitumia bati chakavu ambapo alizitaja idadi yake kufikia Ishirini na  mabati mapya yakiwa mawili ,akiongeza hata yeye ameshangazwa na ujenzi huo

Diwani wa Kata ya Igurubi,Edson Saadan,CCM, amesema  hata yeye anashangazwa na ujenzi wa machinjio kwa kutumia bati chakavu wakati gharama iliyotumika ni kubwa na kwamba suala hilo tayari alilipeleka kwa Mkurugenzi Mtendaji

Kaimu Afisa mifugo wilaya ya Igunga,Reubeni Malawiti ameeleza kuwa machinjio hayo yamejengwa kwa kufuata mkataba uliowekwa na Uongozi wa kata ya Igurubi.

Akizungumzia machinjio hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Igunga,Rustika Turuka ,amesema ujenzi wa machinjio ulifanyika akiwa bado hajahamia Igunga na kuahidi kulifuatilia ili kuweza kujua ni kwa nini ujenzi wa machinjio ulijengwa kwa kutumia bati chakavu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa