Home » » MANISPAA YAAGIZWA KUGAWA MBEGU KWA WAATHIRIKA WA MVUA

MANISPAA YAAGIZWA KUGAWA MBEGU KWA WAATHIRIKA WA MVUA

SERIKALI Wilayani Tabora imeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kununua mbegu za mihogo na kuzigawa kwa waathirika wa mafuriko ambao mashamba yao yamesombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tabora ,Sulemani Kumchaya,muda mfupi  baada ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko na kukagua mashamba yaliyoharibiwa na mvua kubwa ya mawe iliyoambana na upepo mkali na kufanya uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vya Ifucha na Kazima Manispaa ya Tabora.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya uhalibifu huo Kumchaya amemwagiza Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora,Bi Ester Mwangamila kufanya haraka ununuzi wa mbegu hizo ili wananchi wazipande kwa ajili ya kuepukana na baa la njaa.

Pia amemtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kufanya tathimini  haraka iwezekanavyo  ili kubaini idadi halisi ya watu ambao kwa namna moja au nyingine wanahitaji kupewa msaada wa kibinadamu kwa dharura

Mvua hizo ambazo zilinyesha juzi usiku zimefanya uharibifu mkubwa wa mali na mashamba ya mazao ya chakula na biashara ikiwa ni pamoja na kuharibu miundumbinu ya barabara.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa