Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Igunga, mkoani Tabora, Elibariki Kingu,
amewaeleza watendaji wa vitongoji, vijiji, kata na tarafa watakaojiona
hawawezi kufikia malengo ya wilaya hiyo juu ya kuandikisha kaya zilizo
katika maeneo yao kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ifikapo
Julai mwaka huu wajiandae kuondoka.
Amesema malengo ya kitaifa ni kila wilaya kufikia asilimia 30 ya watu
kujiunga na CHF na kwamba Wilaya ya Igunga imedhamiria kuvuka kiwango
hicho kutokana na hamasa na elimu wanayopatiwa wananchi.
Mkuu huyo wa Wilaya (DC) alitoa tahadhari hiyo kwa watendaji juzi
alipozungumza na wakazi wa vijiji vya Mwamashimba na Imalanguvu katika
Kata ya Mwamashimba, Tarafa ya Igurubiha kuhusu kujiunga na mfuko huo.
Alisema jukumu la watendaji ni kuhakikisha kaya zilizo katika maeneo
yao zinajisajili na kupatiwa kadi za CHF, ili iwe rahisi kupata
matibabu katika kituo chochote cha afya ndani ya Wilaya ya Igunga.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment