Home » » WADAU TABORA WAINGIWA HOFU NA TIMU YA RHINO.

WADAU TABORA WAINGIWA HOFU NA TIMU YA RHINO.


Na Hastin Liumba,Tabora
 

 
WADAU wa soka hususani mashabiki wa timu ya soka ya Rhino Rangers ya
mkoa wa Tabora wameingiwa hofu na kukata tamaa juu ya mwenendo wa timu
hiyo kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
 
Wakizungumza baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya timu hiyo na JKT
Mgambo ya Tanga iliyoishia kwa sare ya goli 1-1 iliypoigwa uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi,walisema timu yao wenda ikateremka daraja.
 
Baada ya mechi hiyo mashabiki na wadau mbalimbali walikusanyika
vikundi vikikundi uwanjani humo wakijadili hali hiyo huku wengine
wakidai uongozi wa Rhino Rangers,TAREFA na benchi la ufundi
wameshindwa kazi.
 
"Hapa lipo tatizo siyo bure.....inaonekana hakuna umoja wa kuijenga timu
haiwezekani timu icheze mechi tatu nyumbani isishinde hata moja kuna
jambo hapa tumechoshwa sana na hizi hujuma."alisema mdau
aliyejitambulisha kwa jina la Mwene.
 
Aidha wakizungumza kwa jazba wadau hao walisema jambo lililowazi ni
wadau na mashabiki kutokushirikishwa ipasavyo ili kuisaidia timu hiyo.
 
Walisema hadi sasa timu haieleweki inachocheza ,hakuna sapoti yoyote
toka kwa wadau,TAREFA na uongozi.
 
Timu hiyo imecheza mechi tatu nyumbani ambapo imecheza na JKT Oljro
ikaishia kwa sare ya goli 2-2,ikafungwa na Coastal Union kwa goli 1-0
na kutoka sare tena na JKT Mgambo goli 1-1.
 
Akizungumzia hali na mwenendo wa timu yake kocha mkuu wa timu ya Rhino
Rangers Jumanne Chale alisema matokeo hayo ni mwanzo wa kujipanga na
mchezo mwingine ujao.
 
"Ni kweli tumepoteza pointi nyingi nyumbani....lakini kuisha kwa mchezo
huu ni mwanzo wa kujipanga na mchezo ujao. "aliongeza.
 
Timu hiyo ina kibarua kigumu kwani hadi sasa inashika nafasi ya pili
toka mkiani,huku ikitarajiwa kucheza mechi ngumu na timu ya Yanga FC
na timu yenye hamasa ya mashabiki Mbeya City.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa