Home » » ULYANKULU KUNUFAIKA NA USHURU WA TUMBAKU

ULYANKULU KUNUFAIKA NA USHURU WA TUMBAKU

WATANZANIA wanaoishi eneo la makazi ya wakimbizi la Ulyankulu, wataanza kunufaika na ushuru wa zao laTumbaku ambao walikuwa hawaupati baaba ya kuvunjwa kwa Kata zilizokuwa ndani ya eneo hilo.

Akizungumza nao,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua,Mh.John Kadutu,amesema utaratibu unafanywa ili nao waanze kunufaika na ushuru wa zao hilo kwa vile wanachangia Halmashauri kupata mapato kupitia ushuru huo unaorudishwa kwenye kata kwa ajili ya maendeleo.

Kadutu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ichemba,amesema wananchi wa eneo hilo wanalima sana zao hilo na ni jambo zuri nao kupata ushuru wa zao hilo kwa ajili ya maendeleo ya eneo lao baada ya kuikosa kwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa Kadutu ushuru wa tumbaku uliokuwa ukitolewa kwenye kata zilizokuwa ndani ya eneo la makazi ya wakimbizi,umekuwa ukipatiwa Kata zilizo jirani na eneo hilo ambalo baada ya kuvunjwa kwa Kata zake limekuwa halina wawakilishi katika Baraza la Madiwani.


Zaidi ya wakimbizi Elfu hamisni wanaishi eneo hilo ambapo Elfu wamepatiwa Uraia wa Tanzania baada ya kuomba wakiishi na watanzania wengine wanaofanya kazi kuwahudumia ikiwemo shuleni na katika zahanati.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa