Home » » WAKULIMA 200 KUTOPATA MAZAO MAZURI KUTOKANA NA KUKOSA PEMBEJEO ZA RUZUKU

WAKULIMA 200 KUTOPATA MAZAO MAZURI KUTOKANA NA KUKOSA PEMBEJEO ZA RUZUKU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WAKULIMA Mia Mbili katika Kata ya Itetemia,Manispaa ya Tabora hawatapata mazao mazuri kutokana na kukosa pembejeo za Ruzuku.

Diwani wa Kata hiyo,Haruna Kurwa,amesema wakulima hao kati ya Mia nane wenye mashamba kwenye Kata yake,wamekosa mbolea ya Ruzuku kutokana na kukosa sifa ya kukopesheka.

Amesema hali hiyo imewafanya wasilime kwa kutumia mbolea kwa vile ya kununua ni gharama kubwa kwao na hivyo hawatapata mazao mazuri.

Diwani huyo amebainisha kwamba kutokana na kukosa mbolea ya ruzuku,wakulima hao mazao hayapo katika hali nzuri ukilinganisha na wakulima waliopata mbolea ya ruzuku.

Kwa upande wake Afisa Kilimo na Mifugo wa Kata hiyo,Bw.Cornelius Massawe,amesema ukiachilia mbali tatizo la wakulima hao mia mbili,wanatarajia kuvuna mazao na kujitosheleza kwa asilimia themanini na tano endapo hali ya hewa itaendela kuwa nzuri kama ilivyo sasa.
 Amebainisha kwamba kama wakulima hao mia mbili wangepata mbolea ya ruzuku walikuwa na uhakika mkubwa w akujitosheleza kwa chakula kwenye kata yao ukilinganisha na miaka mingine walipokuwa wakiomba msaada wa chakula.
Kata ya Itetemia ni mojawapo ya Kata zenye Vijiji katika Manispaa ya Tabora ambapo msimu uliopita ilishindwa kujitosheleza kwa chakula na kupewa msaada wa chakula kutoka Serikalini.

1 comments:

T.G.M DESIGNER said...

i am one of the follower of these blog ya mkoa, but i wonder in each blog there is only one post, why

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa