Home » » AMUUA MKE WAKE!

AMUUA MKE WAKE!

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Hastin Liumba,Igunga
  
JESHI la polisi wilayani Igunga mkoani Tabora linamshikilia Athuman
Kiula (49) kwa tuhuma za kumuua mke wake.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Suzani Kaganda akizungumzia tukio
hilo alisema lilitokea mwezi machi 26,mwaka huu katika mtaa wa
hospitali wilayani humo.
 
Kamanda Kaganda alisema mtuhumiwa anatuhumiwa kumpiga mke wake
Magdalena Isaya (34) na kitu chenye ncha kali nyuma ya kichwa.
 
Kamanda huyo alifafanua kuwa mtuhumiwa na mke wake walianza ugomvi wao
wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji wakinywa.
 
Alisema baada ya kuzozana wakiwa kilabuni walirejea nyumbani ambapo
mwanaume aligoma kuingia ndani kulalandipo mke wake ambaye alifariki
alfajiri ya leo (jana) saa 12:00 aliingia ndani kulala.
 
Aidha kamanda huyo alisema marehemu ilipofika majira ya saa nne usiku
ikiwa ni saa moja baada ya wawili hao kurejea nyumbani, alitoka nje
kumuangalia mume wake.
 
Alisema mke alipotoka nje mume wake alimvizia na kumpiga na kitu
chenye ncha kali nyuma ya kichwa ambapo alidondoka chini na kupoteza
fahamu.
 
Aidha aliongeza majirani waliingilia kati na kumchukua mke wake na
kumkimbiza hospitalini kupatiwa matibabu na ilipofika alfajiri ya leo
alifariki dunia.
 
Kamanda Kaganda aliongeza mtuhumiwa huyo alishikiliwa na polisi kwa
kosa la kujeruhi lakini sasa wanamshikilia kwa tuhumza za mauaji ana
atafikishwa mahakani muda wowote baada ya upelelezi kukamilika.
 
Hata hivyo kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni kosa na kutaka
matatizo yote ya ndoa yana taratibu zake kwa mujibu wa sheria za ndoa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa