Kamanda wa Polisi wilaya ya Tabora OCD Samwel Mwampashe akizungumza na wananchi wakati wa tukio hilo la kusikitisha lililotokea na kupoteza maisha ya watoto hao. |
Katikati alijishika kichwani ni Paul Daniel ambaye baba wa watoto hao walipoteza maisha akiangalia maiti za watoto wake hao wawili muda mfupi mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo maswali mengi yalizuka baba huyo alikuwa wapi wakati watoto wanateketea kwa moto ndani ya nyumba. |
Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya alifika eneo la tukio mapema wakati Kikosi cha Zimamoto kikimalizia uzimaji wa moto na kuwatoa watoto hao ambao tayari walikuwa wamekwisha kufa. |
Huyu mama na mtoto walisalimika katika tukio hilo la moto ambao walikuwa kwenye vyumba vingine |
Baadhi ya Samani ziliteketea vibaya kwa moto huo. |
Na Hastin Liumba,Tabora
WATOTO wawili wa familia moja mjini Tabora, wamefariki dunia baada ya
kuteketezwa kwa moto ndani ya nyumba walimokuwa wamelala kutokana na
hitilafu ya umeme.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 01:30 asubuhi katika mtaa wa Ulaya,
Manispaa ya Tabora na mbali ya vifo vya watoto pia mali mbali mbali
ziliteketea kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleman
Kumchaya aliwataja watoto waliofariki kuwa ni Daniel Paul miaka 8 na
Emmanuel Paul mwenye umri wa miaka 3 wote kwa pamoja wameungulia ndani
ya nyumba hiyo.
Kumchaya amesema tukio hilo limetokea wakati baba wa watoto hao akiwa
ameenda stendi kupokea wageni na kuwaacha watoto wake ndani wakiwa
wamelala chumbani.
Kwa upande wake baba wa watoto hao Paul Daniel alisema yeye amepata
taarifa ya tukio baada ya kupigiwa simu na wapangaji wenzake kwamba
sehemu ya chumbani kwake kunaungua moto, hivyo awahi haraka.
Alisema baada ya kufika nyumbani hapo alikuta umati mkubwa wa watu na
baada ya kuingia ndani alikuta kila kitu kimeungua na moto na baadaye
akaelezwa watoto wake pia wameteketea kwa moto na miili yao
imechukuliwa na polisi.
Paul alieleza kuwa wakati tukio linatikea alikuwa ameenda stendi
kumpokea mtoto wa dada yake na ndipo akapigiwa simu kwamba nyumbani
kunatukio, nyumba inawaka moto.
Shuhuda wa tukio hilo Amina Said alisema watoto hao walikutwa wamekufa
chini ya meza sebuleni ambapo inasadikiwa walikimbilia hapo ili
kujaribu kuokoa maisha yao labda, lakini masikini wapi bwana.
Kamanda wa pisi mkoa wa Tabora Suzan Kaganda amethibitisha kutokea kwa
vifo hivyo na kusema jeshi hilo linaendelea na upelelezi kubaini
chanzo cha tatizo .
0 comments:
Post a Comment