Na Hastin Liumba,Tabora
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuzima mitambo ya
kurusha matangazo ya Televisheni ya mfumo wa utangazaji wa Analojia
mwishoni mwa mwezi huu.
Akiongea kwenye warsha iliyohusisha wadau katika hotel ya Orion
mwenyekiti wa kamati ya uzimazi Fredrick Ntobi alisema baada ya zoezi
la uzimaji kukamilika mwezi Februari 2014 awamu ya lili itaanza mwezi
machi 31 mwaka huu.
Alisema maandalizi yote ya uzimaji yameshakamilika kwa mikoa ya Tabora
na Singida kwa awamu ya pili.
Ntobi alifafanua kuwa elimu kwa wadau ya mfumo wa utangazaji kwa njia
ya Dijitali imekuwa ikiendelea kutolewa kwa kiwango cha kuridhisha kwa
asilimia 20 kati ya watu asilimia 24 wanaoendelea na matumizi ya
matangazo ya televisheni ya Analojia.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mabadiliko haya hayatahusu
matangazo kwa njia ya utangazaji wa Satelaiti,Waya (Cable) na Redio.
Aidha alisema mamlaka imeagiza watoa huduma za kusambaza ving`amuzi
walioko mkoa wa Tabora kuhakikisha kunakuwa na ving`amuzi vya kutosha.
Alisema mamlaka pia imeshafanya ukaguzi katika mji wa Tabora na
wamejiridhisha kuwepo ving`amuzi vya kutosha na wamehakikishiwa baadhi
ya ving`amuzi zaidi ya 500 viko njiani vitawasili Tabora muda wowote.
Hata hivyo alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Tabora wasitupe TV zao za
Analojia bali wanunue Ving`amuzi ili kupata matangazo ya Dijitali.
Home »
» TCRA KUKATA MAWASILIANO YA TV TABORA.
TCRA KUKATA MAWASILIANO YA TV TABORA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment