Home » » WACHIMBAJI DHAHABU NZEGA WAANDAMANA.‏

WACHIMBAJI DHAHABU NZEGA WAANDAMANA.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
 Wachimbaji wadogo walitimua mbio kuwepa mabomu ya machozi katika eneo la machimbo lililofungwa pembeni ya mgodi wa Resolte Ltd wilayani Nzega.
 Kijana ambaye hakufahamika jina lake akiwa amezidiwa baada ya kujeruhiwa kwenye vurugu hizo.


JESHI la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limetumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu yaliyolenga  kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited wilayani Nzega.

Awali mkuu wa wilaya ya Nzega Bituni Msangi aliyafunga machimbo hayo kwa mdai kuwa mgodi huo umemaliza muda wake na kwamba wachimbaji hao hawana kibali.

Maandamano hayo yalizuka majira ya saa….. ambapo baada ya kukaribia katika eneo la machimbo ambako maandamano ghafla polisi waliibuka na kuanza kurusha mabomu kuwatawanya.

Taarifa zinasema maandamano hayo yaliitishwa na mbunge wa jimbo la Nzega Dkt Hamis Kigwangalla ambaye kabla ya kuanza kwa maandamano hayo alifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzega ndogo ili kujua mstakabali wa wachimbaji hao.

 Aidha kamishana wa madini nchini Paul Masanja hivi karibuni aliwazuia wachimbaji hao kufanya shughuli za kuchumba kwa kile kilichotajwa kuwa wamevamia eneo hilo.

Kufuatia malalamiko ya wachimbaji hao kuondolewa bila kujali gharama waliozotumia walimwomba mbunge wao aridhie maandamano hadi katika eneo la machimbo.
Hata hivyo kabla ya mkutano wao kufanyika ndipo maandamano yakaanza na polisi waliamua kutumia nguvu kubwa ya mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao walikuwa wakitumia mawe kurusha kwa askari polisi.

Katika  na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa