Home » » WAKAZI 25,250 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SIKONGE.

WAKAZI 25,250 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SIKONGE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Hastin Liumba,Sikonge
 
WAKAZI 25,250 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SIKONGE.
 
ZAIDI ya wananchi 25,250 wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora
wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa maji safi na salama.
 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa alisema hayo kwenye kilele cha
maadhimisho ya wiki ya maji iliyofanyika kimkoa katika kata ya
Kiloleli, wilayani Sikonge.
 
Mwassa alisema mradi huo utahusisha vijiji vya Kiloleli ,Kanyamsenga,
Ukondamoyo, Lembeli,Imalampaka,Mtakuja na maeneo yaliyo jirani.
 
Aliongeza serikali itaendelea kutekeleza malengo muhimu yaliyowekwa
kupitia program ya maendeleo ya maji na yale ya jumuiya za kimataifa
juu ya huduma za usambazaji maji na hatua ya kuyafanya miradi yetu
kuwa endelevu.
 
Mwassa alifafanua licha ya serikali kuendelea kutekeleza program ya
maendeleo ya sekta ya maji ya mwaka 2006 hadi 2025 kwa kufikia
asilimia 90 kwa maeneo ya vijiji na asilimia 100 kwa wakazi wa
mjini,bado wataalamu walitakiwa kufanya kazi zao kwa uadilifu.
 
"Wataalam ningependa kuwaomba kufanya kazi zenu kwa weledi,uadilifu na
kwa kuzingatia maslahi ya taifa."aliongeza.
 
Aidha alizitaka halmashauri zote mkoani Tabora kuweka utaratibu
kuendeleza teknolojia ya uvunaji maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya
majumbani,matumizi ya taasisi kama shule,vituo vya afya,hospitali na
zahanati.
 
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na serikali kuweka
jitihada zake katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama
bado alikumbusha wananchi hao kutumia maji hayo kwa malengo sahihi na
kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
 
Pia alizitaka ofisi zote za bonde la kati na bonde la ziwa Tanganyika
kushirikiana na ofisi za halmashauri kuboresha usimamizi wa rasilimali
za maji na kubaini maeneo mapya yanaweza kujengwa mabwawa.
 
Aidha alionya wananchi,taasisi binafsi na na taasisi za serikali
kutolimbikiza madeni ili kutoa mamlaka husima kujiendesha ipasavyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa