Home » » Asasi yaanzisha Operesheni Okoa mazingira

Asasi yaanzisha Operesheni Okoa mazingira

ASASI ya Uhai Mazingira kwa kifupi ‘UMA’ Wilayani Sikonge imeanzisha operesheni maalumu itakayosaidia kuokoa uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.
Hayo yalibainishwa  na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Bi.Athega Ismail katika hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya utunzaji mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji yaliyoambatana na zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Pangale wilayani Sikonge.
Amesema mradi huo ambao utatekelezwa katika vijiji vyote vya kata za Pangale, Tutuo na Chabutwa wilayani Sikonge umelenga kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji katika maeneo yao sanjali na upandaji miti kwa kila kaya.
Amesema wameamua kujikita katika shughuli ya utunzaji mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji baada ya kushuhudia vitendo vya uharibifu wa mazingira vikizidi kuongezeka siku hadi jambo ambalo athari zake ni kubwa sana kwa viumbe hai akiwemo mwanadamu.
Ili kufanikisha zoezi hilo, Bi. Ismail ameomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika mafunzo watakayoendesha katika kata hizo ili utekelezaji wa mradi huo uweze kuwa na tija katika maeneo hayo kwa faida ya vizazi vyao.
Uzinduzi wa shughuli za asasi hiyo ulioongozwa na Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi. Hanifa Selengu ambapo miti zaidi ya elfu moja ilipandwa katika kata ya Pangale.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa