Na Hastin Liumba,Tabora
SERIKALI imewataka wahitimu wa chuo cha utumishi wa umma (TPSC) tawi
la Tabora na Singida kufanya kazi kwa weledi uadilifu na mafunzo
waliyopata yawe nyenzo kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa lengo
la kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina
Kombani alisema hayo kwenye mahafali ya 18 ya chuo cha utumishi wa
umma tawi la Tabora yaliyohusisha pia tawi la Singida.
Kombani aliwaeleza wahitimu hao ni wakati wao sasa kuwa watendaji
wazuri wawapo kazini kwani wakati wa kuonyesha tofautii kati ya
aliyemalizia chuo cha utumishi wa umma Tanzania na ambaye hajapitia
chuo hapa.
"Ni muda sasa wa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu
za utumishi wa ummma......katika kuendeleza majukumu kwa ufanisi kwa
kuonyesha uwezo wa kumudu majukumu,uadilifu na kutoa huduma bora kwa
wananchi."aliongeza.
Hata hivyo aliasihi wahitimu hao kuacha kufanya kazi zao kwa mazoea na
kuachana na hali hiyo itasaidia serikali kupata matokeo makubwa sasa
ya 'Big Results Now'.
Waziri Kombani alitoa wito kwa wahitimu ambao hawajapata kazi kwenda
kutumia elimu yao vyema kwa kutafuta kazi ambazo zitawaletea maendeleo
binafsi na nchi kwa ujumla.
Waziri huyo aliwataka wahitimu pia kwenda kuwa kioo cha jamiihuko
waendako na kwamba serikali inatarajia kuwa wahitomu wenye mwanga bora
kqwa jamii na aliwakumbusha kuwa macho na ugonjwa hatari wa ukimwi
kwani unaendelea kumaliza nguvu kazi ya taifa.
Aidha aliongeza serikali itaendelea kuajiri wahitimu wanaosoma chuo
cha utumishi wqa ummaTanzania kulingana mahitaji yake.
Awali mtendaji mkuu wa huo cha utumishi wa umma Tanzania Said Nassor
alisema chuo kina mpango wa kufanya upanuzi wa kuanzishwa tawi jipya
jijini Mbeya kuanzia muhula wa pili 2014,kuongeza vyumba vya kompyuta,
madarasa na maktaba ili kukidhi m,ahitaji.
Nassor alifafanua hadi kufikia mwaka 2012/2013 chuo kilikuwa na
wanafunzi wapatao 24,954
Home »
» FANYENI KAZI ZENU KWA WELEDI, UADILIFU-KOMBANI.
FANYENI KAZI ZENU KWA WELEDI, UADILIFU-KOMBANI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment