Home » » PSPF YAZIDI KUWEKEZA KATIKA ELIMU ILI KUBORESHA ELIMU NCHINI

PSPF YAZIDI KUWEKEZA KATIKA ELIMU ILI KUBORESHA ELIMU NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  Meneja wa PSPF mkoa wa Tabora Peter Rushaki mwenye (fulana nyeusi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya chuo na wakufunzi.

  Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ualimu Tabora wakiuliza maswali kwa meneja wa PSPF mkoa wa Tabora Peter Rushaki.
Na Hastin Liumba,Tabora

MFUKO wa Pensheni (PSPF) umeweka bayana mpango wake wa kuboresha elimu nchini kwa kuwekeza katika elimu na ikiwa ni njia yake ya kuwafikiwa jamii kwa ukaribu zaidi.
 
Licha ya mfuko huo kutoa mafao mengine mengi kupitia mpango wa uchangiaji wa lazima unaowalenga watumishi wa umma na ule wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambao unawahusisha watu walio kwenye sekta isiyo rasmi, mfuko huo sasa umedhamiria pia kuwekeza zaidi kwenye sekta ya elimu nchini.
 
Meneja wa PSPF Mkoa wa Tabora Peter Rushaki alisema hayo wakati akiongea na wanafunzi 490 wa chuo cha ualimu Tabora.
 
Wanafunzi waliohudhuria ni wa Diploma mwaka wa kwanza 175 na wanafunzi wa daraja la 3A 315.
 
Rushaki alisema taifa lolote lenye maendeleo thabiti ni lazima
liwekeze kwenye elimu na PSPF kwa kutambua hilo na kuthamini mchango wa walimu na sekta ya elimu wanaunga mkono jitihada za serikali katika kuwekeza kwenye elimu.
 
Rushaki aliongeza kuwa PSPF inadhamini na kujenga vyuo vya elimu kama ilivyo kwa Chuo Kikuu cha Dodoma.
 
Aalisema kuwa kwa sasa PSPF wameongeza mafao mapya matatu likiwemo fao la Uzazi, Ujasiliamali na fao la
elimu.
 
Alitaja mafao mengine ya zamani kuwa ni fao la
uzeeni, ulemavu, kifo, mazishi, wategemezi lisilo na kikomo, kujitoa na uzazi.
 
Mengine ni fao la kufukuzwa kazi, elimu, ujasiliamali, mikopo kwa waastaafu lisilo na riba na mikopo ya nyumba kwa wanachama na wadau mbalimbali.
 
Katika hatua nyingine meneja Rushaki aliwaomba na kuwashauri wanafunzi wa chuo hicho kujiunga na mfuko wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari ili kujiwekea akiba na kupata mafao nono hapo baadae.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa