Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imewaahidi wachimbaji wadogo wa Kitongoji cha Mwanchina,
wilayani Nzega, Tabora kuwatafutia eneo la kuchimba pamoja na kuwaagiza
waunde vikundi vitakavyoweza kupatiwa leseni.
Akizungumza na wachimbaji wadogo juzi, Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Steven Masele, alisema serikali imesikia tatizo hilo na
ufuatiliaji unafanyiwa kazi, ili waweze kupata eneo maalumu la kuchimba
dhahabu, ili waendelee na shuguli zao za kujipatia kipato.
Aliwataka wachimbaji hao kuteua watu watano watakaokuwa wawakilishi
wao ambao wataungana na serikali ya wilaya na mkoa katika kukaa vikao
mbalimbali vya kutatua tatizo hilo, ikiwa na kutengewa eneo la
kuchimba.
Masele alisema baada ya kukamilisha zoezi hilo wachimbaji hao
waunde vikundi vitakavyoweza kupewa leseni ya kuchimba dhahabu katika
maeneo watakayopewa.
“Sisi kama serikali na wizara dhamira yetu ni kuhakikisha
wachimbaji wadogo wanapatiwa leseni kutokana na makazi yao wanayoishi
na zoezi hilo lazima litengenezewe utaratibu mzuri, lengo ni kutoa
migogoro,” alisema.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa, alisema kilio cha
wachimbaji hao kimesikika hadi kusababisha Naibu Waziri wa Nishati na
Madini kuwasili kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment