Na Hastin Liumba,Igunga
SERIKALI Mkoani Tabora na Shinyanga imetoa agizo kwa wakulima wa
wilaya ya Igunga mkoani Tabora kuendelea na shughuli za kilimo huku
ikiimalisha ulinzi na usalama katika mashamba yao.
Aidha imewapiga marufuku wafugaji wa wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga kuvuka na kulishia mifugo yao katika eneo la wilaya ya
Igunga.
Kauli hiyo imefuatia baada ya kuuawa kwa wakulima wanne katika
mapigano ya wafugaji na wakulima yaliyo tokea March 29 katika
kitongoji cha Magogo kata ya Isakamaliwa wilayani Igunga.
Mapigano hayo yalisababisha watu 20 hawajulikani walipo na watu zaidi
ya 150 wameachwa wakiwa hawana makazi baada ya kuchomewa nyumba zao na
wafugaji watokao wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Kamati za ulinzi na usalama ya mikoa ya Tabora na Shinyanga iliketi
kikao chake mpakani mwa wilaya ya Igunga na Kishapu mkoani Shinyanga
nakufikia maamuzi hayo ya kutoa ruhusa kwa wakulima kuendelea na
shughuli za kilimo huku wafugaji hao wa jamii ya Kitaturu kupigwa
marufuku kufanya shughuli zao wilayani Igunga.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mkuu wa mkoa wa
Tabora Fatma Mwassa alisema serikali itahakikisha wakulima wanafanya
shughuli zao huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi kwenye mpaka wa
wilaya hizo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kamati hizo mbili zimefikia muafaka wa
kutatua mgogoro huo ikiwa na wale wote waliohusika na mauaji,uhalibifu
wa mali watafikishwa katika vyombo vya dola kujibu tuhuma zitakazo
wakabili.
Aliwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali yao kutokana na
matokeo hayo watayaona ndani ya siku saba zijazo kuanzia leo na
kuongeza wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa kwa viongozi wao
.
Aidha Fatma Mwassa alimlalamikia Mkuu wa wilaya ya Kishapu Willson
Makumbuka kwa kushindwa kutatua mgogoro ikiwa na kuonesha upendeleo
katika maamuzi yake bila kutambua yeye ni kiongozi wa ngazi za juu
aliyeteuliwa na Rais.
Mwassa alilaani kitendo hicho cha mkuu ya Kishapu na kuongeza
atajadiliwa katika vikao vya ndani dhidi ya maamuzi yake aliyoyafanya
hadi kupelekea kuwaachia watuhumiwa ikiwa na kuachia mifugo iliyokuwa
chini ya ulinzi.
''Mkuu wa wilaya ya Kishapu kutoa maamuzi ndani ya eneo la Igunga ni
makosa,kuachia watu wanao tuhumiwa na vurugu za wakulima ni makosa na
kuvaa mgororo wa Kitaturu ni makosa ulinesha ushujaa wa wananchi wa
Kishapu..... tutakujadili katika vikoa vya ndani'' alisema Fatma Mwassa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Lutunga akitaja mambo saba
yaliyotekelezwa katika zoezi hilo ni pamoja na wafugaji kutoendesha
shughuli zao za kifugaji wilayani Igunga, huku wakulima wakipewa
ruhusa ya kuendelea na kilimo wilayani Igunga.
Alisema azimio la tatu wahalifu wote wa mauaji na uharibifu wa nyumba
zilizochomwa moto wakamatwe ndani ya siku saba kuanzia sasa ikiwa na
kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya wilaya ya Igunga pamoja
na wilaya ya Kishapu.
Nassor alisema azimio la tano na sita ni kutoa Elimu kwa wananchi kwa
pande zote mbili dhidi ya mipaka hiyo ikiwa na muafaka wa kuunda Tume
ya uchunguzi ya watu tisa kila mkoa ilikubaini nini chanzo cha mauaji
hayo.
Aidha Edward Lucas,Rajabu Athumani,Abdullahaman Mrisho waliiomba
serikali kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa wale wote watakao
bainika kuhusika na mauaji hayo ikiwa na uhalibifu huo bila kujali
vyeo vyao ili wakulima waweze kuendelea na shughuli zao pamoja na
sheria kuchukua mkondo wake.
Home »
» WAKULIMA IGUNGA WAREJEA MASHAMBANI
WAKULIMA IGUNGA WAREJEA MASHAMBANI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment