SERIKALI Mkoani Tabora na shinyanga imetoa agizo kwa wakulima wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora kuendelea na shuguli za kilimo huku ikiimalisha ulinzi na usalama katika mashamba yao na kuwapiga marufuku wafugaji wa wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga kuvuka na kulisha mifugo yao katika eneo la wilaya ya Igunga.
Kauli hiyo imefuatia baada ya kuu awa wakulima wa tano katika mapigano ya wafugaji na wakulima yaliyo tokea March 29 katika kitongoji cha Magogo kata ya Isakamaliwa wilayani Igunga huku watu 20 hawajulikani walipo nay a watu zaidi ya 150 wakiwa hawana makazi baada ya kuchomewa nyumba zao na wafugaji waisho wilaya ya kishapu.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma mwasa amesema kuwa serikali itahkikisha wakulima wanafanya shuguli zao kaulinzi wa Jeshi la polis ikiwa na mpaka huo kulindwa kwa muda kadhaa ilikuepusha madhara yanayo weza kujitokeza.
Mkuu huyo amesema kuwa mkuu hizo mbili zimefikia muafaka wa kutatua mgogoro huo ikiwa na wale wote waliohusika na mauaji,uhalibifu wa mali watafikishwa katika vyombo vya dola kujibu tuhuma zitakazo wakabili.
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Lutunga akitaja mambo saba waliyo ya kutekeleza zoezi hilo ni pamoja na wafugaji kutoendesha shuguli zaoza kifugjiwilayani Igunga huku wakulima wakapewa ruhusa ya kuendelea na kilimo chao ndani ya wilaya ya Igunga.
Amesema kuwa azimio la tatu wahalifu wote wa mauaji na uhalibifu wa nyumba wakamatwe ndani ya siku saba kuanzia sasa ikiwa na kuimalisha ulizi na usalama katika maeneo hayo ya wilaya ya Igunga pamoja na wilaya ya Kishapu ilikudhibiti hali hayo.
Mkuu huyo Ally Nassoro alisema azimio la tano na sita ni kutoa Elimu kwa wananchi kwa pande zote mbili dhidi ya mipaka hiyo ikiwa na muafaka wa kuunda Tume ya uchunguzi ya watu tisa kila mkoa ilikubaini nini chanzo cha mauaji hayo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment