Salumu Abel Muhunda mkazi wa Kata ya Cheyo manispaa ya Tabora amejeruhiwa vibaya na kundi la Majambazi ambayo yalimvamia wakati akiuza dukani huko eneo la Mwanga Shop ambapo majambazi hayo yalivamia yakiwa na bunduki na kufyatua risasi hewani huku yakimjeruhi kwa kumpiga mapanga na nyundo kichwani na baadae kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Muhunda ambaye kwasasa amelazwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ni mmoja kati ya watu walioathirika na matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha unaofanywa na majambazi hayo ambayo hufanya unyama huo kila siku na kwasasa takribani miezi mitatu mfululizo eneo la manispaa ya Tabora waathirika wakubwa ni wafanyabishara ya maduka madogo ya mitaani pamoja na M-pesa.
Credit: Kapipi
0 comments:
Post a Comment