Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Hastin Liumba,Tabora
POLISI TABORA YAENDELEA NA OPERESHENI ZAKE.
JESHI la polisi mkoani Tabora limendelea na operesheni zake kukomesha
uhalifu ikiwa na kufanikiwa kukamata wahalifu na vitu mbalimbali
vilivyoporwa.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Tabora ACP Juma Bwire alisema
hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
ACPBwire alisema katika operesheni hiyo endelevu jeshi la polisi
limefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu wakiwa na vitu mbalimbali
ikiwemo baruti 168 za milipuko,Gauge mbili za kupimia baruti.
Alitaja vingine kuwa ni Bhangi gramu 50,Runinga aina JVC moja,box tatu
kubwa na mbili ndogo zenye vitu mbalimbali mchanganyiko dukani,mikuki
miwili,nyundomoja,tindo moja na vyumba mbalimbali vya kuvjunia
makufuli.
Katika matukio mengine mawili tofauti polisi mkoani hapa limawasaka
watu wanaosadikiwa kuwa majambazi ambao mnamo mwezi april mosi,maeneo
ya kata ya Cheyo walivamia nyumbani kwa Sayuni Abel (20) na kupora
vitu na fedha ambazo bado haijaulikana thamani yake.
Alisema tukio hilo polisi inawasaka watatu ili wafikishwe
mahakamani,huku mwezi april 2 huko wilayani Nzega barabara ya
Shinyanga-Nzega gari lenye namba za usajili za T 985 CMU lililokuwa
likiendeshwa na Samweli Daud (29) lilipinduka na kuua abiria mmoja.
Alisema tukio hilo abiria Kamilu Mchilu mkazi wa jiji la Mwanza (56)
alipoteza maisha huku wengine watano ambao majina yao hayajafahamika
wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega chanzo cha
ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi.
Hata hivyo kaimu kamanda ACP Bwire alitoa wito kwa wananchi mkoani
Tabora kuacha mara moja kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume
cha sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment