Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Hastin
Liumba,Sikonge
HALMASHAURI
ya wilaya Sikonge mkoa wa Tabora inatarajia kutumia kiasi cha sh milioni 500
kuboresha huduma za maji katika kipindi mwaka 2013/2014.
Kaimu
mhandisi wa maji wilaya ya Sikonge Jaffar Wibonela alisema kwenye taarifa yake
kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa kwenye ufunguzi wa gati la Maji la
kijiji cha Utyatya wilayani humo.
Wibonela
alisema fedha hizo zinatarajia kuboresha huduma za maji katika vijiji na mji wa
Sikonge.
Alisema hadi
sasa halmashauri imeshapokea kiasi cha sh milioni 300 kati y ash milioni 500
zilizotengwa.
Mhandisi huyo
alifafanu kwa kazi ambazo zitafanyika kwa kipindi hicho ni kujenga kisima
kipya,kujenga nyumba ya mitambo,kununu na kusimika mitambo mipya na kujenga
magati mapya manne.
Aliongeza
kazi nyingine ni kupanua mtambo wa maji mjini Sikonge,kukarabati njia kuu ya
kupandisha maji,kununu na kufunga mita kwa wateja 200 na kununua mtambo wa
dharura.
Mhandisi
huyo alisema hadi sasa kazi ambazo zimeshafanyika ni magati ya maji manne
yamejengwa,mtambo mmoja wa dharura umenunuliwa ambao hadi sasa unafanya kazi.
Aidha
aliongeza kuwa kazi nyingine iliyofanyika ni kujenga nyumba ya mitambo ambayo
imeshakamilika na ujenzi wa kisima kipya ambacho kimeshakalika.
Hata hivyo
mhandisi huyo alisema kazi ambazo zimepangwa lakini bado hazijafanyika ni
ununuzi na usimikaji mitambo kazi ambayo mzabuni alishapatikana.
Aliongeza
kuwa kazi nyingine ambayo itafanyika ni kufanya matengenezo ya njia kuu ya
kupandisha maji kazi ambayo inasubiri usimikaji wa mitambo.
0 comments:
Post a Comment