Na Hastin Liumba,Tabora
WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI.
WATU wawili wamefariki Dunia katika matukio mawili tofauli mmoja kwa
kutumbukia chooni na mwingine kwa kufa maji wakati akioga.
Katika tukio la kwanza mtoto John Mwapwani, alifariki Dunia baada ya
kutumbukia choni alipoenda kujisaidia katika Mtaa wa Skanda,Kata ya
Chemchem,Manispaa ya Tabora.
Kwa Mujibu wa Baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitaja kwa jina moja la
Mwapwani,alisema mtoto wake alienda kujisaidia baada ya kuamka majira
ya saa moja asubuhi na alipochelewa kurudi walianza kumtafuta.
Wakati wakiendelea kumtafuta mtoto huyo mmoja wa watu wanaoishi Nyumba
alipo mtoto huyo alienda kujisaidia na kukuta Ndala za Mtoto zikiwa
ndani ya Choo na alipoangalia kwenye shimo la maji taka lililo ndania
ya choo aliona mwili wa mtoto John na akatoa taarifa Polisi na
walifanikiwa kuutoa kuutoa mwili kwa uchunguzi zaidi.
Katika tukio la pili Mtoto Said Maulid (12) alifariki Dunia baada ya
kuzama kwenye shimo la kufyatulia matofali lililokuwa na maji wakati
akioga na wenzake katika kata ya Ipuli,manispaa ya Tabora.
Kwa mujibu wa majirani wa mtoto huyo walisema Said akiwa na wenzake
wakioga kwenye shimo linalotumika kuchimba udongo wa
matofali,alizidiwa na kushindwa kuogelea baada ya kufika kina kirefu
na kufa maji na wenzake kukimbia huku wakipiga kelele kuomba msaada.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi,Peter
Ouma,amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema Polisi walifanya
kazi yao ya kusaidia na wananchi kuitoa miili ya marehemu na kwamba
uchunguzi zaidi unaendelea.
Home »
» WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI.
WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment