Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAAJIRI nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwachagulia watumishi
kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na pia wameaswa kupeleka
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kuondoa usumbufu
wanapostaafu.
Akizungumza kwenye semina iliyohusisha viongozi na watumishi wa
wilaya zote saba za Mkoa wa Tabora, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa
Tabora, Steven Bushir, alisema mtumishi ndiye mwenye uamuzi wa kujiunga
na mfuko autakao.
Alisema utaratibu wa kuwapangia watumishi kujiunga na mifuko ya jamii
umepitwa na wakati na ulishafanyiwa marekebisho ambapo hivi sasa
mwajiriwa anachagua mwenyewe mfuko wa kujiunga nao.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) washiriki walielezwa toka
kuanzishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni watumishi milioni 22
wamejiunga.
Akitoa mada kwenye semina hiyo, Meneja wa Rasilimali Watu wa SSRA,
Teophory Mbilinyi, alisema lengo ni kupokea kero zinazowakabili
wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mbilinyi aliongeza kuwa SSRA ni chombo ambacho kimeanzishwa na
serikali kwa ajili ya kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze
kutoa huduma bora ikiwemo kutoa mafao yao kwa wakati kwa waastafu.
Hata hivyo, meneja huyo alisema kila Mtanzania mwenye uwezo wa
kufanya kazi anashauriwa kujiunga na mfuko wowote wa hifadhi ya jamii.
Mbilinyi alibainisha awali hakukuwa na udhibiti kwenye mifuko hiyo na
hivyo mifuko iliendesha shughuli zao bila kusimamiwa, hali ambayo
alisababisha kuwepo urasimu katika kuwajibika.
Chanzo;;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment