Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu
wawili waliokamatwa wakimiliki silaha mbili za kivita na sare
zinazotumiwa na jeshi la nchi jirani ya Burundi bada ya kutiwa hatiani
kwa kosa la mauaji.
Waliohukumiwa ni Charles Ngwandu (Mpikachai) na Shaban Mabala (Mwanamswaya).
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Amir Mruma, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.
Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili Edward Mokiwa na
Juma Masanja, ulidai Oktoba 27, mwaka 2008, saa 2 asubuhi, eneo la
Isenefu wilaya ya Uyui mkoani hapa, washitakiwa waliteka mabasi mawili
yaliyokuwa na abiria T 273 AMT mali ya kampuni ya Suden Classic na T 153
AQC mali ya kampuni ya Comb Truck.
Walidai katika tukio hilo walifyatua risasi tano na kumuua papo hapo
abiria mmoja Athumani Mohamed, na mwingine Shaban Masoud alifia
hospitali ya Mkoa Kitete. Pia Hawa Said ambaye alikuwa ni miongoni mwa
abiria alifariki kwa mshutuko baada ya kusikia milio ya risasi.
Akitoa utetezi wake kabla ya kutolewa kwa huduma huyo, Mpikachai
alidai ni mwathirika wa Ukimwi huku mwenzake akidai anasumbuliwa na
ugonjwa wa Pumu.
chanzo; Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment