Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi mkoani Tabora, linawashikilia watu saba kwa tuhuma
za kumuua askari polisi wawili mwishoni mwa Aprili katika eneo la
Ussoke, wilayani Urambo wakati wa tukio la ujambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),
Suzan Kaganda, alisema hadi sasa watu saba wamekamatwa wakihusishwa na
mauaji ya askari F5179 PC Jumanne na G3388 PC Shaban.
Kamanda Kaganda alisema watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na mauaji ya
askari hao baada ya kuhojiwa wakitoka sehemu mbalimbali nchini.
“Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa waliowaua askari hao Aprili 28,
mwaka huu kwa kuwapiga risasi wakati walipokuwa wakienda kukabiliana na
tukio la ujambazi,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Kaganda, watuhumiwa hao wanatoka Urambo,
Mwanza, Tabora Mjini na Ukerewe huku akibainisha kwamba baadhi ya
watuhumiwa hao walikutwa na silaha aina ya pistol glock 17 yenye namba
TZ Car 91968wa na magazini yenye risasi tano.
Alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote kwa vile upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment