Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAAMBUKIZI ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa wajawazito yamepungua kutoka asilimia 3 hadi 2.3.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la EGPAF
Mkoa wa Tabora, Alphaxard Lwitakubi, alipozungumza na waandishi wa
habari na kueleza kuwa wajawazito walioweka wazi hali zao ni asilimia
63.
Alisema kati ya walioweka hali zao wazi wapo waliopatiwa dawa za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo, Lwitakubi alisema ni
kukosa ushirikiano upande wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na
upimaji VVU.
Changamoto nyingine aliyoitaja ni wajawazito kujifungulia nyumbani,
waliogundulika na maambukizi kutorudi vituoni, walezi na wazazi
kutopeleka watoto walioathirika katika vituo vya afya
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment