Home » » DIWANI WA IPULI AMSHUKIA DC

DIWANI WA IPULI AMSHUKIA DC

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DIWANI wa Ipuli, Waziri Mlenda, amemtaka Mkuu wa Wilaya, Suleimani Kumchaya, asiingilie masuala ya ugawaji wa viwanja katika kata hiyo kwani anatakiwa afuate taratibu, sheria na kanuni za ugawaji viwanja.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, alisema  Kumchaya sio kazi yake ya kusimamia mgogoro wa viwanja, na hapaswi kulazimisha halmashauri igawe viwanja kwa wananchi.
‘Mimi ni Diwani wa Ipuli, nasema kutopewa nafasi ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata yangu hiyo ni kunijengea sifa mbaya kwa wananchi.
“Mkuu wa wilaya anapaswa atoe mawazo ya kuwajenga wananchi na sio kuiponda kamati ya Uongozi na kuichafua kwa kuwalainisha wananchi kwa maneno ambayo hayahusiki katika mikutano inayofanyika katika kata hii,” alisema.
Alisema katika ugawaji huyo Mkuu wa Wilaya anatakiwa kuangalia kwa makini kuna wananchi 1,136 na viwanja vinavyopimwa ni 646 kwa mpangilio huo itakuwa mgumu kutokana na viwanja kuwa vichache na wananchi kuwa wengi.
Alitoa wito wa wananchi wa Ipuli kuwa wavumilivu katika ugawaji wa viwanja kama walivyozungumza kwenye mkutano uliopita kabla hajafika Mkuu wa Wilaya  huyo katika mkoa huo
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa