Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFANYAKAZI wa afya wa Kijiji cha Mbola, mkoani Tabora,
wameishukuru Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kutokana na
teknolojia ya huduma ya mawasiliano inayowawezesha kutoa huduma za
afya kwa wigo mpana.
Wafanyakazi hao walipata mafunzo ya namna ya kutumia teknolojia ya
huduma ya afya kupitia simu iitwayo COMCARE, iliyoanzishwa kwa msaada
wa Dagiba ambayo inapatikana kupitia simu za smart phone zenye
‘application’ maalumu inayowawezesha wafanyakazi wa afya kukusanya
takwimu za wagonjwa na kutuma ripoti kwenye vituo vya afya.
Akizungumza wakati wa mafunzo, mmoja wa wafanyakazi wa afya, Amina
Wakasuvi, alisema teknolojia hiyo itawawezesha kufuatilia kazi
zinazofanywa na wafanyakazi wa afya katika maeneo mbalimbali na
wafanyakazi hao wataweza kutuma ripoti zao kwa wakati kila siku kupitia
mtandao wa Airtel.
“Tunawashukuru Airtel kwa ubunifu huu na huduma ya vifurushi vya
intaneti vya bure vinavyotuwezesha kufanya kazi zetu kwa wakati,”
alisema.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi, alisema kwa miaka
mitatu sasa Airtel imewekeza katika kuleta mapinduzi ya kupatikana kwa
huduma kwa jamii hususani katika maeno ya vijiji vya Tabora kwa
kushiriki katika mradi wa Millennium Village kama mtoaji mkuu wa
huduma za mawasiliano.
Katika mradi huo, Airtel inatoa njia ya mawasiliano kwa kuwezesha
jamii inayoishi katika maeneo ya pembezoni kupata huduma za afya.
Wafanyakazi wa afya katika maeneo hayo wameunganishwa na mtandao wa
kisasa unaowapatia huduma ya intaneti na simu na kurahisisha kazi zao
pindi wakiwa kazini.
Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa mradi wa Millennium Village,
Dk. Gerson Nyadzi, alisema mtandao wa 3G wa Airtel umewawezesha kwa
kiasi kikubwa kufikia maeneo ya vijijini ambako huduma ni duni na
haba.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment